26.9 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 5, 2023

Contact us: [email protected]

Lowassa amshukuru Rais Samia kwa chanjo

Na Mwandishi Wetu

Mbunge wa Jimbo la Monduli, Arusha, Fredrick Lowassa, amemshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada na  kuhakikisha chanjo ya ugonjwa wa Corona inapatikana haraka akianza kusambaza dozi 1,050,000 nchi nzima.

 Lowassa amesema yeye amekuwa mtu wa 972 kupata chanjo ya Covid 19 katika Wilaya ya Monduli iliyozinduliwa wilayani humo na Mkuu wa Wilaya, Frank Mwaisumbe, Agosti 3, 2021.

Amesema  kuna watu wachache  wanajaribu kubeza, lakini wakumbuke hii siyo kazi rahisi hata kidogo,ukizingatia msimamo wa nchi yetu ulivyokuwa  dhidi ya janga  hili hapo nyuma.

“Dunia nzima imeamini kwamba njia  sahihi na ya kisayansi ya kujikinga na janga hili la Corona ni hizi chanjo zilizothibitishwa na WHO (World Health Organisation).

“Ndugu na marafiki zetu wengi wanafariki kila siku kwa janga hili la Covid-19, unadhubutu vipi kumshawishi mtu asichanje wakati haujampatia mbadala  wowote wa kujikinga?

“Kipekee, nimshukuru sana Rais wetu Mama Samia Suluhu Hassan kwa  jitihada kubwa sana, hasa tukizingatia kwamba amekuwa Rais ndani ya muda mchache sana”, amesema Lowassa.

Pia amewapongeza wahudumu wa afya wa Monduli na nchi nzima kutokana na kuhangaika kila siku kuhatarisha maisha yao ili kuokoa ya wengi.

“Naomba Wanamonduli na Watanzania wenzangu tuwapuuze, tukajilinde dhidi ya Janga hili, lakini zaidi tuendelee kumuunga mkono na kumtia moyo Rais,” ameeleza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
580,000SubscribersSubscribe

Latest Articles