32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Iddy Chilumba: Korosho ni tegemeo langu

korosho-1024x650

NA MWANDISHI WETU, Dar es Salaam

“SASA hivi biashara yangu imekuwa na ninazungumzia oda ya tani za korosho sio pakiti za korosho tena .”

“Sasa hivi biashara ni nzuri na wateja wameongezeka hivyo ninaishukuru Ai

.rtel  wezesha kwa kuniona ,kuthamini wazo langu  na kunifanya  nifanikiwe kibiashara leo hii.”

Haya ni maneno ya kijana  Iddy Chilumba (24) mkazi wa Mtwara ambaye ni mmoja kati ya vijana waliofanikiwa kibiashara kupitia progaramu ya Airtel fursa iliyoanzishwa na kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel mwaka mmoja uliopita .

Historia yake

Akielezea historia yake Chilumba  anasema alizaliwa na kukulia mkoani Mtwara lakini baba yake mzazi alifariki akiwa na mwezi mmoja.

Hakupata bahati ya kumjua baba yake alilelewa na mama yake tu ambaye ni mkulima. Maisha yake ya kusoma yalikuwa ya shida sana kutokana na mama yake kutokuwa na kipato kikubwa ilimlazimu  kufanya kazi za kibarua akitoka shule ili kupata ada ya kuendelea na masomo.

Iddy alimaliza shule ya msingi na kufaulu kuweza kuendelea na sekondari lakini alivyomaliza kidato cha nne hakuweza kufaulu vizuri.

Mama yake mdogo alimsaidia kumsomesha kozi  ya kompyuta baada ya kumaliza alipata kazi kwenye duka la vifaa vya shule na   alifanya kwa muda wa miaka  miwili na kuamua  kuacha yeye mwenyewe kwa kuwa siku zote ndoto yake ni kujiajiri mwenye na kuwasaidia vijana wenzake. Biashara ya Korosho

Anasema aliamua kufanya biashara ya kubangua korosho ili kumsaidia mama yake na ndugu zake.

Ili kufanya biashara yake kwa uhakika zaidi Mwaka 2015 alienda kwenye mafunzo ya kubangua korosho yaliyo kuwa yakitolewa na SIDO kwa muda wa miezi miwili.

Anasema Mafunzo hayo yamekuwa ni nguzo kubwa kwa Iddi kwani ameweza kujua namna bora ya kutengeneza korosho.

Hata hivyo kutokana na kipato chake kidogo  Chilumba alishindwa kununua vifaa vya kubangua korosho ili aweze kuboresha biashara yake hivyo alipaosikia kuhusu Airtel fursa ilimlazimu kujaribu  kuandika mpango kazi wake na alifanikiwa na kupata mafunzo maalumu ya ujasiriamli sambamba na vitendea kazi kutoka Airtel .

Anasema Airtel ilimpa Mashine ya kubangulia Korosho ambayo ilinunuliwa kutoka shirika la viwanda vidogovidogo( SIDO) ,Meza  mbili za kuanikia korosho, mifuko maalumu ya kufungia korosho , mashine ya ‘vaccum seal’ ambayo hutumika kufungia korosho pamoja na Pikipiki ya kusafirishia mizigo.

Iddy Chilumba
Iddy Chilumba

Mafanikio

Akizungumzia jinsi alivyonufaika na programu ya Airtel fursa ambayo kimsingi imemfanya kuwa kijana mwenye mafanikio  hasa kujitegemea na kuweza kumudu kuihudumia familia yake.

Mbali na hilo Chilumba ameweza kutoa ajira kwa vijana kadhaa jambo ambalo anajivunia .

Chilumba anajinasibu kuwa malengo yake ni kuwa mfanyabiashara mkubwa wa korosho Mtwara na mikoa   yote Tanzania kwani  anaamini katika ujasiriamali zaidi  na amethubutu kufanya ujasiriamali.

Airtel fursa

Akizungumzia kuhusu progarmu hiyo, Meneja Huduma za Jamii wa Airtel Tanzania,  Hawa Bayumi anasema kuwa  mara nyingi jamii imekuwa ikisikia kuhusu Airtel Fursa  kwa kuona matangazo mbalimbali bila kuwa na elimu na ufahamu sahihi kuhusu  Program hiyo ambayo kimsingi ina tija na imeonyesha mafanikio makubwa kwa vijana wachache walioina fursa hiyo na kuichangamkia.

Bayumi anasema ni  Mradi wa kijamii wenye dhumuni la kuhamasisha vijana, kuwapa nafasi ya kujiendeleza kibiashara na ujuzi utakoawawezesha kuimarisha biashara zao.

Anafafanua kuwa ni mojawapo ya programu ndani ya Kampui ya Airtel iliyoanzishwa takriban mwaka mmoja uliopita ambapo umeweza kunufaisha vijana 4,000 ikiwemo mmoja mmoja na vikundi katika mikoa mbalimbali Tanzania.

Anasema  kupitia programu hiyo  kampuni ilijikita katika kusaidia vijana walio na umri wa miaka 18 hadi 24, na anasema kuwa, Airtel imeweza kuwasaidia vijana kujiajiri wenyewe  na kuendeleza biashara  zao ambazo awali zilikuwa zikiendeshwa bila utaalamu wowote wa biashara,vitendea kazi duni,ukosefu wa maeneo stahiki ya kufanyia biashara sambamba  na  mitaji midogo.

Bayumi anakwenda mbali zaidi na kueleza kuwa vijana hawa huweza kusaidiwa na Airtel kwa kufuata utaratibu uliowekwa ambapo kijana mjasiriamali hutakiwa kuandika mpango kazi wake na kisha kuuwasilisha kwa kampuni iliyopewa dhamana  na Airtel wenyewe.

Baada ya hapo mawazo ya mpango kazi wa vijana mbalimbali huchambuliwa  na  kufanya uchaguzi wa mawazo mazuri ya biashara ambao baada ya hapo kifuatacho ni  kuwaita wahusika ambao huandaliwa mafunzo ya ujasiriamali ambapo baada ya kufuzu hupewa vifaa.

“Naomba nieleweke kwamba Airtel huwa hatutoi fedha bali tunachokifanya n kumwezesha mjasiriamali kupata vitendea kazi ambavyo humwezesha kufanya shughuli zake kisasa zaidi,” anasisitiza Bayumi.

Bayumi anatanabaisha kuwa kupitia programu hiyo Airtel imeweza kutoa mwanga wa maisha na kuondoa pengo la ajira katika taifa hivyo kutoa tumaini la maisha katika jamii kwa maana ya kwamba wao si watoa huduma tu bali hutumia faida yake katika kuhakikisha jamii inapata maendeleo.

“Pamoja na mambo yote wahusika wote hufuatiliwa kuhakikisha kila mmoja husimama  kwa miguu yake ili kukuza biashara kupitia progarmu hii ya Airtel fursa,” anahitimisha Bayumi

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles