23 C
Dar es Salaam
Wednesday, September 18, 2024

Contact us: [email protected]

Kampuni za kigeni zinavyoshindana biashara mafuta, gesi Afrika – 4

1395182180739

NA FARAJA MASINDE,

SAFARI ya kampuni hizi zaidi ya 500 zinazowania nishati barani Afrika inaendelea ambapo leo tunaangalia nchini, Morocco, ambako huko kuna kampuni kubwa ya ndani ya Akwa Group S.A. ikiwa na makao makuu yake katika mji wa Casablanca.

Akwa Group ambayo ilianzishwa mwaka 1959Afriquia SMDC, ukiacha masula ya Nishati pia iko kwenye Nyanja za Utalii, hoteli, mawasiliano, majengo makubwa, huku ikiwa na kampuni nyingine zinazojihusisha na mazao ya gesi.

Ukiacha hiyo pia kuna kampuni nyingine kama, Kosmos&Cairn Energy, BP-Statoil, Chevron (Marekani), Circle Oil Plc zinazojihusisha na usakaji wa nishati nchini humo.

Hata hivyo licha ya kupitia kwenye ghasia za kisiasa bado kuna kampuni nyingi ambazo zinaenda kuwekeza nchini humo ikiwamo kufanya utafiti uchimbaji wa mafuta na gesi, eneo ambalo limekuwa tegemeo la uchumi wa nchi hiyo.

Kuna kampuni nyingine kama, Challenger Ltd inayojihusisha na uchimbaji, Dana Petroleum ya Uingereza inayofanya kazi ya kutafiti, EGAS ambayo ni kampuni ya taifa, ENGC, Petrosalam, SEGAS LNG nyingine ni VOG ya Ugiriki inayofanya kazi ya kutafiti

Pia kuna, EGPC, ENGHC na East Mediterranean Gas Co. inayomiliki bomba la mafuta la Arish-Ashkelon, ikiwa ni kampuni ya ubia baina ya Mediterranean Gas Pipeline Ltd (inayotokana na kampuni Evsen Group of Co inayomiliki asilimia 28, Merhav ya Israel (asilimia 25), PTT (asilimia 25), EMI-EGI LP (asilimia 12), na Shirika la Petroli la Misri (Egyptian General Petroleum Cor lenye asilimia 10 ya hisa kwenye bomba hilo.

Tukiangalia upande wa nchi jirani ya Tunisia kampuni zilizowekeza nchini humo ni pamoja na ETAP ambayo iko chini ya serikali ikisimamia shughuli zote za nishati ya mafuta na gesi kwa niaba ya serikali; Rigo Oil Co Ltd, Cygam, SEREPT, Carthago Oil Co, Exxoil, MARETAP, SMIP, TOPIC Energy, Voyageur Oil and Gas Cor, Joint Oil, Range Petroleum Ltd, BG Group Plc, ENI S.P.A.

PA Resources AB, Preussag Energie GmbH, PNRCo, Perenco, Winstar Resources Ltd, Lundin Petroleum, Atlantis Holdings Norway AS, Storm Ventures International Inc, na Candax Energy Inc.

Tukija hapo Cameroon kampuni zilizowekeza humo ni pamoja na Dana Petroleum plc ya Uingereza, Madison Cameroon Oil&Gas Ltd, Soft Rock Oil&Gas Ltd, Perenco ya Ufaransa, Kosmos Energy na ile ya umma ya Société Nationale des Hydrocarbures.

Upande wa Congo Brazzaville, kuna kampuni zilizowekeza ni Perenco, Total, Chevron, SNPC, Eni, SOCO, World Natural Resources, Africa Oil & Gas, Petrovietnam, National Co of Oils of Congo, PA Resources Congo S.A., Afrimel Italgru, Cameron France S.A.S, Engen Congo, Enterprise Petrol ere du Congo, Ministered des Hydocarbures et des Mines Service des mines et da la Geologie, Oil Tools Services Ltd, SDV Oilfield Congo, Societé Nationale de Recherches et d’Exploitation Petroliere, Société Nationale des Pétroles du Congo, na Zetah M&P Congo SARL.

Usikose kusoma sehemu ya mwisho wiki ijayo, Maoni &Ushauri | 0653045474

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles