26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

ICC yaitaka Sudan kuruhusu wachunguzi kuwafikia mashahidi

 KHARTOUM, SUDAN

Mwendesha mashtaka wa mahakama ya kimataifa ya kushughulikia kesi za jinai ICC ameitolea mwito serikali ya Sudan kutekeleza wajibu wake kivitendo katika suala la kutafuta haki kwenye jimbo la Darfur.

Mwendesha mashtaka wa ICC, Fatou Bensouda ameitaka serikali ya Sudan kuonesha kwa vitendo uwajibikaji wake katika suala la haki kwa watu wa jimbo la Darfur, kwa kuanza na hatua ya kuwaruhusu bila ya vipigamizi, wachunguzi wa mahakama hiyo kuwafikia mashahidi, maeneo ulikofanyika uhalifu pamoja na ushahidi mwingine katika eneo hilo kubwa la magharibi mwa Sudan.

Mwendesha mashtaka wa ICC Fatou Bensouda

Katika maelezo yake mbele ya baraza la usalama la Umoja wa Mataifa aliyoyatowa kwa njia ya vidio, Fatou Bensouda amesema kwamba hatilii shaka uaminifu wa maafisa wa ngazi za juu kutoka serikali ya mpito ya Sudan lakini amesisitiza kwamba suala la wachunguzi kuruhusiwa kuingia Darfur ndilo hasa wanalolitarajia wahanga,na ndicho kitu ambacho Sudan kwa uungaji mkono wa baraza la usalama inachopaswa kukisimamia.

Mgogoro katika jimbo la Darfur ulizuka baada ya waasi kutoka jamii ya wasudan weusi wenye asili ya kutoka nchi za Kusini mwa jangwa la Sahara na Afrika ya kati,kuanzisha uasi mwaka 2003 wakilalamikia ukandamizaji wanaofanyiwa na serikali ya Sudan mjini Khartoum iliyohodhiwa na waarabu.

Serikali ya rais wa wakati huo, Omar al-Bashir ilijibu uasi huo kwa kuanzisha kampeini kubwa ya mashambulizi ya anga ya mabomu na kupeleka wanamgambo waliofahamika kama Janjaweed katika eneo hilo. Inaarifiwa kwamba wanamgambo hao walifanya mauaji ya watu wengi pamoja na ubakaji.

Zaidi ya watu 300,000 waliuwawa na wengine milioni 2 na laki 7 waliachwa bila makaazi.

Mahakama hiyo ya ICC iliyoko mjini The Hague Uholanzi ilimshtaki, al Bashir kwa makosa ya uhalifu wa kivita na mauaji ya halaiki akituhumiwa kwamba ndiye aliyepanga kampeini ya mashambulizi katika jimbo la Darfur. Rais huyo wa zamani wa Sudan sasa yuko jela tangu jeshi lilipomuondowa madarakani kufuatia shinikizo kubwa la waandamanaji mnamo mwaka 2019.

Maafisa wengine wawili waandamizi waliokuweko katika utawala wa Bashir,waliotuhumiwa na mahakama hiyo ya ICC  kwa uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya ubinadamu, nao pia wanashikiliwa mjini Khartoum.

Maafisa hao ni Abdel-Rahim Muhammad Hussein, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani na ulinzi katika kipindi kirefu cha mgogoro huo pamoja na Ahmed Haroun, aliyekuwa kiongozi wa ngazi ya  juu wa masuala ya usalama na baadae akawa kiongozi wa chama tawala cha rais Bashir.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles