25.2 C
Dar es Salaam
Monday, April 22, 2024

Contact us: [email protected]

Huyu ndiye Tiffany Trump, mtoto wa Rais mpya wa Marekani

Tiffany akimpongeza baba yake Donald Trump kwa kushinda Urais
Tiffany akimpongeza baba yake Donald Trump kwa kushinda Urais

Tiffany Trump (23) ni binti wa Donald Trump kutoka kwa mke wake wa pili Marla Maples, mwigizaji wa zamani na nyota wa Televisheni.

Kwenye mitandao ya kijamii, Tiffany hupendelea sana Twitter na Instagram akiwa na wafuasi zaidi ya 236,000 na sifa yake kubwa ikiwa ni mara kwa mara kutuma ujumbe wa kifahari na picha zakuvutia.

Mrembo huyo ambaye amefuzu chuo kikuu hivi karibuni, alikuwa hana kawaida yakujitokeza sana kwenye kampeni za Donald Trump, lakini alisifiwa sana na baba yake kwa kutoa hotuba nzuri sana wakati wa kongamano kuu la chama cha Republican, ambapo alisema babake ni mtu mwenye sifa za kuwasaidia na kuwahimiza wengine.

tiffanyt9-e1436834467977
Tiffany Trump

Chakufurahisha zaidi ni kwamba mchumba wake anayetambulika kwa jina la Ross Mechanic (21), ni mwanachama wa chama cha Democrat na amekuwa akitoa ushirikiano sana katika kumnadi Hillary Clinton mpinzani wa Trump kwenye mitandao ya kijamii wakati wa kampeni za kuwania urasi wa Marekani.

Tiffany ni mwanamitindo mashuhuri ambaye amefanya kazi na wanamitindo wengi maarufu nchini Marekani kama vile Kya na Gaïa lakini pia ni mwimbaji mzuri ambaye aliianza kuimba akiwa na miaka 17.

Pampoja na mambo mengine Tiffany ni mtu mwenye kupenda marafiki na mwenye kupenda kushirikian na wengine katika mambo mbalimbali hasa yale ya kijamii.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles