24 C
Dar es Salaam
Thursday, July 25, 2024

Contact us: [email protected]

TB Joshua arejesha utabiri wa ushindi wa Clinton Facebook

index
TB JOSHUA

Utabiri kutoka kwa mhubiri raia wa Nigeria TB Joshua kuwa Hillary Clinton angeshinda urais wa Marekani, umerejeshwa tena baada ujumbe huo kufutwa kutoka mtandao wa Facebook.

Kulingana na barua pepe iliyotumwa kwa BBC na idara ya mitandao ya kanisa la TBJMinistries ilisema kuwa , “ujumbe huo uliondolewa kimakosa na sasa umerejeshwa kwa kuwa hiyo si sera yetu.”

“Siku kumi zilizopita nilimuona rais wa Marekani akishinda kwa kura chache, yule niliyemuona ni mwanamke,” ujumbe huo ulisema.

TB Joshua alikejeliwa kwa wingi kwenye mitandao ya kijamii wakati watu walitambua kuwa ujumbe huo ulikuwa umefutwa, licha ya wafuasi wake wengi katika mitandao ya kijamii bado kumtaja kuwa nabii. Source: BBC

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles