26.4 C
Dar es Salaam
Tuesday, November 26, 2024

Contact us: [email protected]

HUTAMCHUKULIA POA MOBETTO UKIWACHEKI WAREMBO HAWA

Na CHRISTOPHER MSEKENA


MUZIKI wa Bongo Fleva umempokea kwa mikono miwili mwanamitindo Hamisa Mobetto baada ya kuachia ngoma yake ya kwanza Madam Hero, iliyoweka rekodi ambayo baadhi ya wanamuziki nchini wameshindwa kuifikia.

Wimbo huo ulioandikwa na mtunzi Foby na kutengenezwa na Prodyuza C9 Kanjenje, umelenga kumpa hamasa ya kutokata tamaa mwanamke katika kupambana kwa kufanya shughuli mbalimbali za kujikwamua kimaendeleo bila kurudishwa nyuma na changamoto zilizopo katika jamii.

Mwanamitindo huyo ambaye pia ni mwigizaji amejiwekea rekodi ambayo wana Bongo Fleva wengi huwa wanashindwa kuifikisha ya wimbo wake Madam Hero, kusikilizwa na watu zaidi ya  200,000 ndani ya siku moja katika mtandao wa Youube.

Hatua hiyo imemfanya Mobetto awe gumzo kila kona kutokana na wimbo wake kupokelewa vizuri siyo na mashabiki pekee bali mastaa mbalimbali wamejitokeza kumpongeza  kwa kutoa ngoma hiyo huku wengine kuibuka na kumponda wakidai hawezi kuimba na siyo kila mtu anaweza kuwa msanii.

Hamisa amewatumia wanawake wenye mafanikio barani Afrika kama vile Makamu wa Rais wa Tanzania, Samia Hassan Suluhu, staa wa filamu nchini Marekani akitokea Kenya, Lupita Nyong’o, Mama wa Afrika na msanii wa muziki, Yvonne Chaka Chaka na Miriam Makeba.

Swaggaz tumeona tukupe orodha ya warembo ambao muziki kwao haukuwa chaguo la kwanza kama vile anavyofanya Hamisa lakini walipojaribu wakafanikiwa, hadi leo hii ni mastaa wakubwa wa muziki Bongo.

LULU DIVA

Lulu Abbas maarufu katika anga la Bongo Fleva kwa jina la Lulu Diva, mrembo ambaye tulianza kumwona katika vichupa vya wasanii kama ‘Video Vixen’ miaka miwili iliyopita lakini sasa hivi ni staa mkubwa wa muziki akisimamiwa ya Lebo ya Born To Shine AR.

Lulu Diva ambaye hakuaminiwa sana alipoanza kuimba, anasema Hamisa ni mtu anayempa hamasa katika mambo mbalimbali na tayari wana kolabo ambayo wakiitoa itasumbua chati za muziki Bongo.

“Mobetto ni mfano wa kuigwa na wanawake wengi, amekuwa akijaribu kufanya vitu vingi na kufanikiwa, kuna kitu chetu tunakiandaa yaani sijui tukikitoa itakuwaje,” alisema Diva alipochonga na Swaggaz.

VANESSA MDEE

Hakuna anayeweza kubisha kwamba ndiyo msanii namba moja wa kike mwenye mafanikio kwa sasa, amefanikiwa kimuziki licha ya safari yake kuanzia kwenye tasnia ya habari akiwa kama mtangazaji.

Ukimtazama Vee Money, alipotoka mpaka alipo sasa hivi unaweza kukosa sababu ya kumchukulia poa mwanamitindo Mobetto katika safari yake mpya kwenye muziki.

SHILOLE

Zuwena Mohamed ‘Shilole’ yupo kwenye orodha ya wasanii watano wa kike wenye thamani kubwa Bongo, lakini muziki aliuanza kama masihara lakini alipowekeza nguvu akaacha kuigiza na kujikita rasmi muziki.

Hamisa anakanyaga nyayo za Shilole kwa sababu wimbo wake Madam Hero, umetengenezwa na mikono ya C 9 Kanjenje, prodyuza aliyetengeneza wimbo wa kwanza wa Shishi aliomshirikisha Q Chief, Lawama uliotoka miaka sita iliyopita.

GIGY MONEY

Huyu ni mrembo mwingine ambaye anachukia sana kwa sasa ukimtambua kama Video Vixen, anataka afahamike kama msanii wa muziki kwani ngoma zake kama Nampa Papa, Mimina, Kiki ni Gigy na nyinginezo zimemfanya apate shoo kibao kama mwanamuziki.

AMBER LULU

Muziki haukuwa chaguo la kwanza kwa Amber Lulu, tulimfahamu kama mrembo anayependezesha video za muziki lakini alipoingia kwa miguu miwili kwenye muziki sasa hivi hakamatiki kwenye Bongo Fleva.

Amber Lulu, anasema sasa hivi ameamua kuacha matukio yote mabaya na skendo zilizomchafua ili ajikite kwenye muziki kwa sababu sasa hivi ameufanya kama kazi yake ya kudumu.

Hivyo basi ukiwatazama warembo hao wa Bongo, unaweza kuona kuwa Hamisa, anaweza kuja kuwa msanii wa muziki mpaka watu wakaanza kusahau kama ni mwanamitindo kama ataufanya muziki kwa kumaanisha kwani uwezo tayari ameonyesha na mashabiki wamempokea.

Muda utaongea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles