30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Huduma ya M-Pesa yatua nchi za SADC

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

KAMPUNI ya simu za Mkononi ya Vodacom imezindua huduma mpya ya nyongeza ya Vodacom M-Pesa ‘Dunia Kijiji’ inayowezesha kutuma na kupokea pesa katika nchi za Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).

Kampuni hiyo imepanua wigo wake wa Fedha wa Kimataifa (IMT) mpaka katika nchi za Afrika Kusini, Malawi, Zambia, Zimbabwe, Lesotho, Msumbiji, Swaziland na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.  

Mkurugenzi wa M-Pesa wa Vodacom, Epimack Mbeteni. akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma ya M-Pesa kwa Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) ambayo inawezesha kutuma na kupokea pesa katika nchi hizo, jijini Dar es Salaam leo.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa huduma hiyo, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dk. Stargomena Tax, amesema

 hatua hiyo itaboresha uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla.

Aliwataka Watanzania kuitumia vizuri huduma hiyo kujikwamua kiuchumi katika ukanda huo wa SADC.

“Sisi kama serikali tunaona jambo hili lililofanywa na Vodacom ni kubwa na la muhimu katika sekta ya fedha….. tunatambua kwamba sasa hivi nchi iko katika uchumi wa kidigitali, hivyo na sekta ya fedha lazima ifanye kazi kidigitali, niwaombe Watanzania mahali popote walipo ndani na nje ya nchi kutambua kwamba kuna huduma hii hivyo waitumie iweze kuwasaidia kujiletea maendeleo,” amesema Dk. Tax.

Amesema kupitia huduma hiyo Watanzania wanaoishi nje pia watanufaika kwa kuleta fedha zao nchini hasa katika kipindi hiki ambacho Serikali inatoa kipaumbele katika kuvutia uwekezaji na kuhakikisha mazingira ya kufanya na biashara yanakuwa rahisi.

Amesema alipokuwa SADC walianzisha mfumo wa sekta ya fedha jumuishi kwa nchi hizo, hivyo kilichofanywa na M-Pesa ni sehemu ya mpango huo.

“Mbali na ukuaji wa kiuchumi, lakini hatua hii imesaidia mtu mmoja mmoja kwani inarahisisha gharama za kutuma fedha kwani zinamfikia mlengwa kwa wakati,” amesema.

Naye Mkurugenzi wa M-Pesa Tanzania, Epimack Mbeteni, amesema baada ya kufanya vizuri katika ukanda wa Afrika Mashariki sasa wameamua kupanua wigo kwa nchi za SADC.

Amesema safari ya Vodacom M-Pesa IMT ilianza mwaka 2014 kwa kuungana na Kenya, mwaka 2019 kufanikiwa kutuma na kupokea fedha kote Afrika Mashariki na kupokea fedha kutoka nchi zaidi ya 200 duniani.

Amesema huduma hiyo mpya itawawezesha wateja wa Tanzania kutuma malipo kutoka M-Pesa kwenda akaunti zote za benki nchini Kenya, Uganda na Rwanda.  

“Mbali na masuala ya biashara lakini pia mfumo huo umerahisisha kwa wanafunzi wanaosoma nje ya nchi, wagonjwa wanaotibiwa lakini pia hata ndugu na jamaa ambao wanaweza kutumiwa fedha na kupokea,” amesema Mbeteni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles