29.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 11, 2024

Contact us: [email protected]

Huduma za fedha kwa simu za mkononi zaimarika-Utafiti

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Utafiti mpya kutoka kwa kampuni ya Vodafone Group, Vodacom Group, Safaricom na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa (UNDP, United Nations Development Programme) unaonyesha kuwa uenezaji na matumizi fanisi ya huduma za fedha za simu za mkononi yanahusishwa na athari nzuri ya moja kwa moja kwa ukuaji wa Kiwango cha Uchumi (GDP).

Hiyo ni katika masoko yanayokua kwa sababu husaidia biashara kupunguza gharama, kupata mkopo wa kuwekeza na kuwasiliana na wateja ambao hawakuwa na uwezo wa kufikia huduma za fedha hapo awali.

Kwamujibu wa Utafiti wa mfano wa takwimu za uchumi1 – ambao ulichunguza nchi 49 barani Afrika, Asia na Amerika Kusini – ulibainisha kuwa nchi zilizokuwa na huduma fanisi za fedha za simu za mkononi zilikuwa na ukuaji wa Kiwango cha Uchumi kwa kila mtu kwa mwaka cha hadi asilimia 1 zaidi kuliko nchi ambako mifumo ya huduma za fedha za simu za mkononi hazikuwa fanisi au zilikuwa hazijaanzishwa.

“Kulingana na utafiti wa awali wa Benki ya Dunia (World Bank) kuhusu uhusiano kati ya ukuaji wa uchumi na kupungua kwa idadi ya watu wanaoishi katika umaskini, ukuaji huu wa Kiwango cha Uchumi (GDP) kwa kila mtu unamaanisha kuwa nchi zenye huduma fanisi za fedha za simu za mkononi zinaweza kupunguza umaskini kwa karibu asilimia 2.6,” umebainisha utafiti huo.

Uchanganuzi huu ulifanywa kama sehemu ya kampeni ya makampuni ya Africa.Connected, mradi wa kuendeleza ukuaji endelevu kupitia ushirikiano na kusaidia kuondoa tofauti zinazozuia maendeleo katika sekta kuu za uchumi barani Africa.

Matokeo haya ni sehemu ya utafiti mpya, Mifumo Dijitali ya Fedha ya kuwezesha watu wote (Digital Finance Platforms to Empower All), utafiti wa nne uliotayarisha na kuchapishwa chini ya mwavuli wa utafiti wa Africa.Connected.

Sitoyo Lopokoiyit, Afisa Mkuu Mtendaji wa M-Pesa Africa na Afisa Mkuu wa Huduma za Fedha katika kampuni ya Safaricom, alisema:

“Mifumo ya huduma za fedha za simu za mkononi kama vile M-Pesa ni viendeshaji muhimu vya usawa wa kufikia huduma za fedha katika jamii, hali ambayo inaweza kuboresha fursa za maisha ya mtu binafsi na kuwezesha biashara kuanzishwa na kupanuka, na kuleta utajiri na ajira katika uchumi unaokua.

“Ingawa bado kuna vizuizi vya kufikia mifumo hii – ikijumuisha ufahamu wa masuala ya dijitali na ufikiaji wa simu mahiri – na kuikuza – na kiwango cha udhibiti usio sawa kwa watoa huduma za kisasa za fedha katika nchi nyingi,” unabainisha utafiti huo.

Kama sehemu ya utafiti wa Africa.Connected, utafiti wa watumiaji ulifanywa kwa kulenga watumiaji wa huduma ya M-Pesa nchini Kenya na Tanzania na matokeo yake yalibashiriwa kwa nchi ya Ghana na Msumbiji.

Utafiti wa biashara ulifanywa pia nchini Kenya. Utafiti huo ulizingatia umuhimu unaozidi kuongezeka wa huduma ya fedha ya simu za mkononi ya kwanza duniani miaka 15 baada ya kuzinduliwa kwake mwaka wa 2007. Utafiti huu ulikadiria kuwa:

“Watumiaji wa sasa ambao ni milioni 17.6 katika nchi hizi nne hawakuwa na uwezo wa kufikia huduma zozote rasmi za fedha kabla ya kuanza kutumia huduma ya M-Pesa, asilimia 98 ya biashara zilizofanyiwa utafiti zilisema kuwa huduma ya M-Pesa huzisaidia kufanya biashara ambapo faida kuu za huduma ya M-Pesa ni uwezeshaji wa malipo ya haraka na salama na kuwezesha uuzaji wa bidhaa na huduma mtandaoni na
asilimia 95 ya biashara zilizofanyiwa utafiti zilisema kuwa zinatumia huduma ya M-Pesa kwa angalau nusu ya shughuli zake za malipo ya biashara,” unabainisha utafiti huo.

Ulrika Modeer, Naibu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN Assistant Secretary-General) na Mkurugenzi wa Ofisi ya Mahusiano ya Nje na Utetezi (Director of the Bureau of External Relations and Advocacy) katika shirika la UNDP, alisema:

“Usawa wa ufikiaji wa huduma za fedha ni masharti ya mapema na kiwezeshaji muhimu cha kutimiza Malengo mengi ya Ukuaji Endelevu ya Umoja wa Mataifa (UN’s Sustainable Development Goals), ikijumuisha kupunguza umaskini, kukuza ukuaji wa uchumi, kuendeleza ufikiaji wa soko na kuhimiza uwekezaji katika sekta muhimu kama vile elimu, kilimo na afya.

“Lakini muhimu zaidi, ni kuhusu kuwapa watu kipaumbele, kuwapa nguvu zaidi ya kudhibiti pesa zao na kukuza ukakamavu wao. Kuondoa hali za kutengwa kifedha barani Afrika, na duniani, lazima kiwe kipaumbele ikiwa tunatarajia kutimiza lengo la ustawi endelevu wa pamoja kwa ajili ya kila mtu katika dunia bora,” amesema Modeer.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles