MWANAMITINDO maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe, amejitapa na utajiri alionao kwa sasa na kusema kwamba uji wa chumvi aliwahi kunywa mara moja katika kumbukumbu za maisha yake.
Mrembo huyo mwenye mbwembwe nyingi, amedai kwa sasa yeye ni tajiri tofauti na miaka ya nyuma ambayo aliwahi kunywa uji wa mahindi uliowekwa chumvi.
Kupitia akaunti yake ya Instagram, mrembo huyo aliweka picha huku akionyesha vitu vyake vya thamani, ikiwemo gari lake aina ya Range Rover SUV na nyumba yake mpya.
“Katika maisha hakuna kukata tamaa, ninaamini juhudi zangu zimenifikisha hapa kwa sasa, nina vitu vingi vya thamani kwa sasa na nishasahau maisha yale ya uji wa chumvi.
“Kwa sasa siwezi tena kunywa uji wa mahindi wenye chumvi, niangalie kwa sasa nakula soseji, mikate na vitu vingine,” alieleza Huddah.