23.3 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Hospitali ya AMI yafungwa rasmi

HATIMAYE Hospitali ya African Medical Investment Ltd (AMI) maarufu kama Trauma Center ya Masaki Dar es Salaam, imefungwa rasmi na mmiliki wa jengo kukabidhiwa funguo zake.
Hospitali ya AMI na ya gharama ya juu, ilikuwa ikitoa matibabu kwa viongozi wa ngazi za juu wa Serikali, wabunge, mabalozi na wafanyabiashara wakubwa wa ndani na nje ya nchi.
Kufungwa kwa hospitali hiyo ni kutokana na kushindwa kulipa kodi ya pango kwa zaidi ya miezi 26, inayofikia zaidi ya dola za Marekani milioni 1.6, ambazo ni zaidi ya Sh bilioni tatu.
Makabidhino hayo yalifanyika jana hospitalini hapo kati ya Mwakilishi wa Kampuni ya udalali wa Mahakama ya MEM Auctioneers and General Brokers Ltd, Elieza Mbwambwo kwa Meneja wa jengo hilo, Zurfiq Hassanar, dalali huyo wa mahakama alisema hatua hiyo kuhamishwa kwa hospitali hiyo imetokana na uamuzi wa Mahakama Kuu.
“Ninapenda kusema leo (jana), tunakabidhi jengo na funguo zake kwa meneja wa jengo hili kwa niaba ya mteja wetu, wiki mbili zilizopita tulikamata mali baada ya AMI kushindwa kulipa deni kama ilivyoamriwa na mahakama.
“Mahakama Kuu ilichoamuru mali za AMI zikamatwe na kupigwa mnada ili kuweza kulipa deni lao la pango na kisha kuondolewa kwenye jengo na kumkabidhi mmiliki ambaye ni Navtej Singh Bains,” alisema Mbwambo.
Mali zilizokamatwa ni magari matatu ya kubebea wagonjwa (Ambulance), vitanda maalumu vya kulaza na kuwahudumia wagonjwa, gari ndogo aina ya Mark II, mashine mbalimbali pamoja na samahani zilizokuwa zikitumiwa katika jengo hilo.
“Tulipokuja awali tulitoa taarifa kwa ndugu wa wagonjwa wawe wamewaondoa wagonjwa wao na sasa jengo ni jeupe halina mtu ndani, hata mali tilizokamata tutazipiga mnada ingawa tunajua haziwezi kufikia thamani ya fedha zinazodaiwa, maana kwa sasa kuna maombi mengi ya watu wanataka kufungua hospitali hapa,” alisema.
Alisema mashine za CT -Scan, X-ray ni miongoni mwa mali zitakazopigwa mnada huku atakayepanga katika jengo hilo akipewa kipaumbele cha kwanza.
Hatua hii ya kufukuzwa kwenye jengo imefikiwa baada ya mabishano ya muda mrefu ya kisheria baina ya AMI na mfanyabiashara ambaye pia ni mmiliki wa jengo hilo, Navtej Singh Bains.
Taarifa zaidi inasema kwamba, akaunti za benki za hospitali hiyo ya AMI katika Benki ya Exim zilizoambatanishwa na Mahakama zilikutwa zikiwa zimefungwa na fedha zote zikiwa zimetolewa.

Amri ya kufurushwa kwa AMI ilitolewa Mei 7, mwaka huu na kusainiwa na Makamu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa AMI Plc, Theunis Peter Botha, ambaye pia ni Mkurugenzi na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya AMI Tanzania, aliwasilisha ombi Mahakama Kuu ya Tanzania kuwa imefilisika.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles