26.7 C
Dar es Salaam
Monday, March 4, 2024

Contact us: [email protected]

ACT yamlilia Yamola

CHAMA cha ACT – Wazalendo, kimetuma salamu za rambirambi kwa tasnia ya habari nchini na familia ya marehemu Sophia Yamola, kutokana na kifo chake kilichotokea juzi katika Hospitali ya Jeshi Lugalo. Anaripoti Mwandishi Wetu Dar es Salaam.
Rambirambi hiyo imetolewa jana na Mwenyekiti wa chama hicho Taifa, Anna Mghwira, ambaye alisema ni pigo kwa kada nzima ya uandishi wa habari nchini na kutaka waandishi, ndugu na familia ya marehemu kuwa na uvumilivu katika kipindi hiki kigumu kwao.
Mghwira, alisema mbali na Sophia kuwa mwandishi pia alikuwa ni mwanasiasa wa ACT aliyekuwa na uthubutu katika kile alichoamini kuwa ni sahihi kwake.
Alisema chama hicho kimempoteza mpambanaji makini aliyetumia kalamu yake kwa uadilifu, kuhakikisha jamii inapata taarifa sahihi.
“Nimemfahamu wakati wa uchaguzi wa chama chetu pale aliposhinda kuwa mjumbe wa Halmashauri Kuu, lakini wenzangu waliniambia kuwa alikuwa ni sehemu ya wanachama wa awali kujiunga na chama na hakuwahi kuipindisha kalamu yake kwa manufaa ya chama, hivyo atakumbukwa kwa mchango wake,” alisema Mghwira.
Machi 28, mwaka huu Sophia alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya ACT-Wazalendo, akiwa ni miongoni mwa wagombea wachache waliopata kura nyingi kati ya wote.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
584,000SubscribersSubscribe

Latest Articles