29.2 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Hofu iliyopitiliza hushusha kinga za mwili – Msaikolojia

 SARAPHINA SENARA (UoI) -DAR ES SALAAM

MTAALAMU wa masuala ya saikolijia kutoka Chuo Kikuu cha Iringa, Baraka Mushobozi, amesema madhara ya hofu iliyopitiliza kwa binadamu ni pamoja na kushuka kwa kinga za mwili na kuruhusu mwili kushambuliwa na magonjwa. 

Akizungumza na MTANZANIA katika Mahojino Maalum jana, alisema watu wengi wamekua wakisumbuliwa na hofu na bila kujijua wamejikuta wakipata maumivu makali mwilini ambayo hawajui chanzo chake.

“Hofu inaanza kujithihirisha kwenye mwili kwanza, kwa kupata maumivu yasiyoeleweka, kama kuanza kupata maumivu makali ya mgongo au kuumwa na kichwa sana hata anapomuona daktari akajikuta haoni tatizo,”alisema Mushobozi. 

Alisema watu wengi haswa vijana wamekua na hofu kwasababu tu yakuhindwa kutimiza kile walichotarajia, matokeo yake kupata hofu iliyopitiliza. 

“Ukiwa na hofu sana moja ya matokeo yake ni kupata msongo wa mawazo ambao unaweza kusababusha kushuka kwa kinga ya mwili na kupata magonjwa nyemelezi kama mafua na hii ipo kwa wanafunzi wengi wakati wa mitihani,”aliongezea. 

Alisema hofu inaweza pia kusababisha tatizo la kushuka kwa homoni kwa upande wa wanawake na kuchangia tatizo la kushindwa kupata mtoto kwa wale ambao wako kwenye ndoa.

“Kunawakati hata uwezo wa kufikiri unaweza kushuka kwasababu tu mtu anaweza kushindwa kustahimili hofu aliyonayo hivyo kumchanganya katika kutumia akili yake vizuri na kupambanua mambo.

“Hata mtu anavyoweza kupanga mipango yake unaona kabisa ni tofauti kulinganisha na wengine hii inatokana na hofu ambayo tayari ameshakua nayo na kumfanya kushindwa kutumia akili yake vizuri,”alisema Mushobozi.

Aidha ameelezea sababu zinazoweza kupelekea mtu kuwa na hofu,huku akisema wengine huwa na hofu bila kujua hata chanzo chake.

“Tukio lolote linaloweza kufanya mtu kuona kuna hatari fulani ya kutokamilisha jambo hivyo kama litafanya kuona hana uhakika wa jambo, kuna uwezekano wa kupelekea hofu.

“Mazingira yasiyompa uhuru wa kutosha kwenye jambo kulifanya ama kutokuwepo usalama wake katika hayo mazingira kunamfanya mtu kupata hofu kwasababu hana uhakika wa usalama,”alisema. 

Hata hivyo alisema kuna wengine wamekua na hofu kutokana na vina saba vyao, na kujikuta wamekua na hofu na kuanza kuogopa baadhi ya mambo fulani ambayo sio nzuri kwao.

Sababu nyingine inayopelekea hofu ni namna ya mtu anavyofikiri na kutengeneza maana ya mambo fulani, ambayo hayaonekani katika uhalisia wake, jinsi ambavyo mtu fikiri ndivyo anaweza kutengeneza hofu ndani yake.

“Mtazamo wa mtu juu ya jambo fulani unaweza kusababisha pia mtu kupata hofu kwasababu tu tafsiri ya jambo alivyo lichukulia na kupelekea mtu huyo kupata hofu,”alisema Mushobozi.

Alisema hofu ni kitu cha kawaida kwa kila binadamu sema inapozidi kile kiasi kinachohitajika ndio huleta shida na matatizo kwa mtu husika.

Alishauri kumuona mtaalamu wa saikolojia ili kupata ufumbuzi pale mtu anapoona kuwa yuko kwenye hofu inayomsumbua, napia kwa mtu ambae anasumbuliwa na msongo wa mawazo uliotokana na hofu anaweza kumuona daktari ili aweze kupata msaada wa kitaalamu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles