28.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Maalim Seif avuka kigingi cha kugombea urais Zanzibar

 FARAJA MASINDE -DAR ES SALAAM

PINGAMIZI lililowekwa na vyama viwili kumzuia Maalim Seif Sharrif Hamad kugombea urais kwa tiketi ya chama cha ACTWazalendo limeondolewa na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), imempitisha kuwania nafasi hiyo.

Kutokana na hatua hiyo ambayo Maalim Seif sasa anaruhusiwa kuanza kampeni.

Uamuzi huo wa ZEC ulitangazwa jana visiwani humo na Mwenyekiti wa tume hiyo, Hamid Mahmoud Hamid.

“Mimi Hamid Mahmoud Hamid Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi wa Zanzibar nathibitisha kuwa, Tume imekuteua rasmi, Seif Sharif Hamad wa Chama cha ACT kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Zanzibar kwa mujibu wa Sheria.

“Kwa uthibitisho huu Tume ya Zanzibar inakuruhusu kuendesha mikutano ya kampeni kwa mujibu wa sheria, kanuni, miongozo ya tume na ratiba ya kampeni,” alisema Hamid.

Awali, Tume hiyo ilitangaza kuwaruhusu wagombea 16 wa urais wa Zanzibar kuanza kampeni zao Septemba 11, mwaka huu, lakini iliacha kumpitisha Maalim Seif kwa sababu ya kuwekewa pingamizi.

Kutokana na hilo kampeni zilizotangazwa kuwanza jana Ijumaa (Septemba 11) za urais wa Zanzibar, uwakilishi na udiwani, hazikufanyika kwa wagombea kadhaa wa ACT-Wazalendo, akiwemo Maalim Seif ambaye amekuwa akitikisa siasa za visiwa hivyo katika chaguzi takribani zote tangu mfumo wa vyama vingi uanze.

Maalim Seif aliwekewa pingamizi na wagombea urais wa vyama viwili vya upinzania visivyo na ushawishi mkubwa vya Democratic Party (DP) na Demokrasia Makini.

Aidha wagombea wa uwakilishi wa ACT-Wazalendo wengi wao waliwekewa pingamizi zaidi na wenzao wa chama kinachotawala, CCM.

Mapema jana, Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Thabit Idarous Faina, aliwaambia waandishi wa habari kwamba Maalim Seif alipingwa kwa sababu miongoni mwa fomu zake za kuomba uteuzi zilikuwa na makosa, kwa mujibu wa waweka pingamizi. 

Hadi ya saa 4:00 usiku wa Alhamis (Septemba 10), hakukuwa na mwafaka kwenye kikao cha kujadiliana pingamizi hilo katika ofisi za ZEC zilizopo Maruhubi, kando kidogo ya kitovu cha Mji Mkongwe wa Zanzibar, na suala hilo lilipelekwa mbele, ikitarajiwa uamuzi wake kutoka jana. 

Wakati hayo yakijiri, mapema jana wagombea wengine kadhaa wa nafasi za uwakilishi na udiwani wa chama hicho nao pia hawakukabidhiwa vyeti vya uteuzi na ZEC, baada ya kujulishwa kwamba wamewekewa pingamizi na wenzao kutoka CCM.

Chama cha ACT-Wazalendo kimekuwa kikilalamika kuchezewa rafu kwenye uchaguzi huu, ambapo kwenye mkutano wake na waandishi wa habari siku ya Jumatano (Septemba 9), Naibu Katibu Mkuu Nassor Mazrui, alionya dhidi ya kile alichokiita “njama ovu za kuwaenguwa wagombea” wa chama chake.

Kwa mujibu wa ACT Wazalendo katika wilaya nzima ya Magharibi, wagombea wote wanne wa uwakilishi na madiwani wao waliarifiwa kuhusu pingamizi na maofisa wa ZEC saa 11:00 jioni, ikiwa ni saa nzima tangu kumalizika kwa muda rasmi wa kuweka pingamizi. 

Hata hivyo, kama zilivyo siasa za Zanzibar, ni vyama viwili tu ndivyo vinavyotazamiwa kutunishiana misuli kwenye uchaguzi huu – chama kinachotawala cha CCM, ambacho kilitangaza kuanza leo na 

ACT Wazalendo ambao wanajipanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles