27.1 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Mwanafunzi adaiwa kuungua kwa moto wa maajabu

 ELIZABETH KILINDI -NJOMBE

MWANAFUNZI wa kidato cha katika Shule ya Sekondari Madilu iliyopo wilayani Ludewa mkoani Njombe, Roida Mwabena, amejeruhiwa sehemu mbalimbali za mwili wake mara baada ya sare ya shule aliyovaa kuanza kuungua moto wakati akiwa njiani kuelekea shuleni, huku chanzo cha moto huo kikiwa hakijulikani.

Akizungumza na Mtanzania juzi mtoto huyo alisema alishangaa ghafla kuona moto unawaka kwenye mavazi yake jambo lililomfanya kukimbia kurudi kwa baba yake mkubwa.

“Mimi niliona moto unawaka ghafla nikaanza kukimbia kwa baba mkubwa akanitoa sketi akauzima ule moto”alisema mtoto huyo.

Mwalimu Mkuu wa Shule ya Sekondari Madilu, Michael Mwalongo, alisema tukio hilo lilimkuta mwanafunzi huyo saa 12 asubuhi wakati akitoka nyumbani kwenda shuleni. 

“Wakati akiwa njiani kuja shule ndio tukio hilo lilimkuta na ameungua sketi ya shule na sweta, moto ule wasamaria wema walijaribu kuuzima na baadaye wakamleta shule, kumchunguza akawa ameungua na mkono baada ya hapo mzazi akaja kumchukua na pikipiki na kumpeleka kituo cha afya,”alisema Mwalongo.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Kituo cha Afya Madilu, Salmini Magunja, alikiri kumpokea mwanafunzi huyo ambaye alifikishwa hapo kwa ajili ya matibabu huku nguo zake zikiwa zimeungu pamoja kuwa na majeraha ya moto.

“Tulimpokea na kweli na sare za shule zilikuwa zimeungua moto na yeye kuna baadhi ya maeneo ya mwili kidogo ulishika moto, tulimuuliza labda ulitembea na kiberiti alisema hapana na hapa tumempa matibabu ya kawaida kama mtu aliyeungua moto japo hili ni jambo la ajabu mpaka ndugu zake wameshangaa, lakini kwasababu hali yake ni nzuri tumemruhusu aende nyumbani”alisema Magunja.

Baba mzazi wa mtoto huyo, Andrea Mwabena, akizungumza kwa njia ya simu kuhusuana na tukio hilo alisema “hali hiyo ilimkuta asubuhi, hata sisi tunashangaa kwa kweli ndio maana tumekaa tuangalie nini chanzo cha huu moto, kwasababu moto ukianza kuwaka bila chanzo ni tatizo na ukiangali hili tukio la moto ni la kwanza hatujawahi kuona.”

“Yaani na mimi sielewi hili tatizo hadi saizi kwa sababu aliaga vizuri asubuhi akaondoka lakini nikaona baba ake ananipigia simu anasema njoo huku mtoto anawaka moto,”alisema Regina Mnyanga mama wa mtoto huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles