30.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

HIZI NDIZO DALILI ZA MTOTO KUCHOKA SHULE WATOTO

signs-and-symptoms-of-dyspraxia-drugs-inn-com_-1

NA AZIZA MASOUD,

WATOTO wanapozaliwa huwa wanapita katika hatua mbalimbali za makuzi, ikiwa ni pamoja na kukua kimwili na kiakili.

Katika hatua hizo kuna wakati ambao mtoto anafikia umri wa kuanza kujifunza vitu mbalimbali vya nyumbani, vipo vitu ambavyo mtoto anaelekezwa na mzazi, pia kuna muda ambao anahitajika kwenda shule kwa ajili ya kujifunza mambo mbalimbali.

Asilimia kubwa ya wazazi wanaopeleka watoto wao kuanza shule hushawishiwa na watoto wenyewe  pamoja na mzazi kuwa na wazo la kufanya hivyo.

Msukumo wa watoto kutaka kwenda shule  mara nyingi unachangiwa na jamii inayomzunguka, hasa anapokuwa anawaona  baadhi ya marafiki zake ama watu wake wa karibu wanatoka kwenda  shule.

Pamoja na kuwa mtoto anakuwa anapenda mwenyewe, pia kuna umri ambao mzazi unapaswa uhakikishe mwanao anaanza  shule.

Watoto wanapozoea  kwenda shule baada ya muda wanaanza kuchoka, jambo ambalo linawafanya kutoa malalamiko kwa wazazi ili waweze kutengeneza mazingira kuwa yupo mahali asipostahili.

Ukifika wakati huo kila mtoto anakuwa na sababu zake, lakini zipo nne ambazo watoto wengi huzisema kwa wazazi wao.

Wengi huanza kwakusema masomo magumu, kama mzazi unapaswa kutenga muda  kumuuliza kwa undani na kama mtoto wako ni mkubwa, mfano yupo sekondari  muulize ni aina gani ya mada ama masomo yanayomsumbua.

Akishakutajia  ni jukumu lako kumtafutia mtu wa kumsaidia  kumfundisha na kumpa mazoezi madogo madogo mara kwa mara, anaweza akatoka ndani ya familia ama nje, kwakutumia njia hiyo utakuwa umemsaidia  na kumwondolea mtanziko mtoto wako.

Kama mtoto wako ni mdogo na anashindwa  kujielezea ugumu anaokutana nao, panga muda wa kukutana na mwalimu wake  ambaye atakuelezea kuhusu maendeleo ya mtoto na kukushauri njia za kumsaidia.

Mbali na hilo, malalamiko mengine ya wanafunzi ni ya kutompenda mwalimu, hii inatokea endapo kuna mwalimu ambaye hamuelewi darasani ama mwenye utaratibu wa kutoa kazi nyingi, hasa mazoezi ya nyumbani.

Wakati mwingine mtoto akichoka kwenda shule anaweza tu kuja na kukwambia hana amani katika hali nzuri anapokuwa shuleni.

Anapokuwa katika hali hiyo unaweza ukamuacha mpaka muda wa likizo na kumtaka achague sehemu nzuri ya tofauti ambayo angependa kupumzika.

Kwa kutumia muda huo, unapaswa kumwelewesha kuhusu hasara na faida ya kuwa na elimu, huku ukimtolea mifano mibaya ya watu wasiokuwa na elimu na shida wanazozipata.

Watoto pia wana tabia za kulalamikia uchovu asubuhi wanapokuwa wanaamshwa kwa ajili ya kujiandaa kwenda shule.

Akifika katika hali hii jitahidi  kuhakikisha anapata muda wa kutosha wa kulala mchana baada ya kutoka shule, jambo ambalo litamsaidia kupunguza uchovu.

Kutokana na tabia hizo, hakikisha unamfuatilia mtoto kwa ukaribu, mzazi usikubali mtoto wako aingie katika majaribu ya kuona kwenda shule kama sehemu ya adhabu badala ya kuwa faraja kwake.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles