26.3 C
Dar es Salaam
Wednesday, November 27, 2024

Contact us: [email protected]

Hatma ya kina Malinzi Julai 23

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

Hatima ya aliyekuwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania ((TFF), Jamal Malinzi na wenzake wanne kama wana kesi ya kujibu ama la itajulikana Julai 23 mwaka huu.

Uamuzi huo umetolewa leo asubuhi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi, Maira Kasonde baada ya Jamhuri kufunga ushahidi.

Akiiwakilisha Jamhuri Wakili wa Serikali kutoka Tasisi ya Kuzuia nA Kupambana na Rushwa (Takukuru), Leonard Swai alidai kesi ilikuja kwa ajili ya kusikilizwa na wanania ya kufunga ushahidi.

“Mheshimiwa upande wa mashtaka tunaomba kufunga ushahidi kwa upande wetu,”alidai Swai na mahakama ilikubali.

Upande huo ulikuwa na mashahidi 15 waliotoa ushahidi.
Mahakama imeamuru itatoa uamuzi wa kama washtakiwa wana kesi ya kujibu ama la Julai 23 mwaka huu na endapo watakutwa na kesi ya kujibu watatakiwa kuanza kujitetea.

Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Mhasibu wa TFF, Nsiande Mwanga, Meneja wa Ofisi TFF, Miriam Zayumba, Katibu wa shirikisho hilo, Selestine Mwesigwa na Karani wa TFF, Flora Rauya ambao kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 30 katika kesi ya jinai namba 213 ya mwaka 2017.

Washtakiwa wanakabiliwa na mashtaka mbalimbali yakiwamo ya kula njama, kughushi, kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu na utakatishaji wa dola za Marekani 173,335.

Malinzi, Mwesigwa na Nsiande wanaendelea kusota rumande kwa sababu wanakabiliwa na mashtaka ya utakatishaji fedha ambayo hayana dhamana kwa mujibu wa sheria.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles