Nanenane kitaifa kufanyika Simiyu

0
976

Na Christina Gauluhanga, Dar es Saalaam

Maonesho ya Wakulima ‘Nane Nane’ yanatarajiwa kuanza rasmi Julai 28, mwaka huu katika Viwanja vya Nyakabindi, mkoani Simiyu.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 12, Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu, Jumanne Sagini amesema maonesho hayo yanafanyika mkoani Simiyu kwa mara ya pili.

Amesema maandalizi yote tayari yamefanyika ambapo yatafunguliwa rasmi Agosti moja hadi nane mwaka huu na tayari maandalizi yamekamilika ikiwamo maboresho ya miundombinu ya maji na barabara.

“Mwaka jana tulikuwa na washiriki zaidi ya 1,000 lakini kwa mwaka huu wataongezeka kwa sababu ya hamasa ya Maonesho yaliyopita,”amesema Sagini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here