33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Hatima ya rufaa ya Kafulila leo

Aliyekuwa mgombea ubunge Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR- Mageuzi)
Aliyekuwa mgombea ubunge Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR- Mageuzi)

NA JONAS MUSHI, DAR ES SALAAM

HATIMA ya ombi la aliyekuwa mgombea ubunge Kigoma Kusini, David Kafulila (NCCR- Mageuzi), kutaka kufungua upya rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa na Mahakama Kuu Kigoma kuhusu uchaguzi wa jimbo hilo, itajulikana leo.

Mawakili wa Kafulila, Majura Magafu akishirikiana na Mussa Kassim waliwasilisha  maombi hayo Mahakama Kuu wakiomba kuirudisha rufaa hiyo baada ya kutupiliwa mbali na Mahakama ya Rufaa Oktoba 13 mwaka huu.

Kesi hiyo ilitajwa Novemba 3 mwaka huu mbele ya Jaji E.Mrango wa Kanda ya Tabora na ikasikilizwa Novemba15.

Jaji Mrango alipanga kutoa uamuzi wa ombi hilo leo, kujua kama rufaa hiyo itarudishwa au la.

Oktoba 12 mwaka huu, rufaa ya kupinga matokeo ya Jimbo la Kigoma Kusini ilisikilizwa mbele ya Majaji watatu wa Mahakama ya Rufaa, Jaji Benard Luanda, Jaji Salim Mbarouk na Jaji Richard Mziray katika Mahakama Kuu Kanda ya Tabora.

Hata hivyo Mawakili wa Serikali wakiongozwa na Wakili Gabriel Malata waliweka pingamizi kuhusu hati ya rufaa kwamba ilikuwa na kasoro na hivyo rufaa yote ifutwe na isirudishwe tena mahakamani.

Hata hivyo, majaji hao wa rufaa  katika uamuzi, Oktoba 13, 2016 walikataa ombi la mawakili wa Serikali kuitupa rufaa hiyo kwa maana ya mlalamikaji asiwe na uwezo wa kuirudisha kwa hoja kwamba kasoro za hati zinaweza kurekebishwa na kwa kuwa mahakama haijasikiliza hoja za rufaa yenyewe.

Badala yake Mahakama iliondoa rufaa hiyo na mlalamikaji anaweza kuomba kuirudisha upya  rufaa hiyo mahakamani.

Kafulila aliliambia MTANZANIA jana kuwa katika maombi yake kutaka kuingiza rufaa hiyo upya ni ili pia apate fursa ya kuingiza katika Mahakama ya Rufaa fomu za tume No 21B za kila kituo kwa vituo vyote 382 kusomwa matokeo yake kubaini mshindi tofauti na ilivyokuwa katika ngazi ya Mahakama Kuu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles