Na Asifiwe George, Dar es Salaam
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillus Wambura, amesema Jeshi hilo kwa sasa lipo katika uchunguzi dhidi ya mtangazaji wa Kituo cha Redio cha Clouds FM, Ephraim Kibonde na mwenzake, Gadna Habash wa Times FM, ambao wameachiwa huru kwa dhamana.
Kamanda Wambura aliliambia MTANZANIA jana kwamba baada ya uchunguzi huo, iwapo watapatikana na hatia, hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao, ikiwa ni pamoja na kufikishwa mahakamani.
Kwa mujibu wa Kamanda Wambura, Kibonde na Gadna wanadaiwa kutenda makosa matano, ikiwamo kusababisha ajali, kukimbia, kutotii amri halali ya Polisi, kukimbia na trafiki ndani ya gari, kutoa lugha chafu kituoni pamoja na kukataa kupima ulevi.
Alisema watangazaji hao waliyatenda makosa hayo siku ya Jumamosi saa 12 asubuhi, katika eneo la Makumbusho, ambapo Kibonde akiwa anaendesha gari walilokuwa wamepanda aliligonga gari la raia mmoja wa kigeni (Mzungu) na kukimbia.
Jana MTANZANIA lilishuhudia askari wa usalama barabarani wakiwa wameongozana na Kibonde pamoja na raia huyo wa kigeni katika eneo la tukio ambapo walikuwa wakipima ajali hiyo.
wanatakiwa kujua kuwa kwenye sheria hakuna umaaarufu, lazima watii sheria bila shuruti