23 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Hatima madeni ya Serikali kutikisa Bunge

Bunge
Bunge

Na Bakari Kimwanga, Dodoma

MJADALA kuhusu azimio la kuliomba liidhinishe kufutwa au kusamehe hasara na madeni yaliyotokana na upotevu wa mali na fedha, yenye thamani ya Sh bilioni 10.8, unatarajiwa kulitikisa Bunge leo.

Hatua hiyo inatokana na mvutano ulioibuka mwishoni mwa wiki iliyopita miongoni mwa wabunge, kundi moja likitaka azimio hilo lipite na wengine wakipinga hatua hiyo wakisema ni sawa na ufisadi.

Hasara hiyo imetokana na sababu mbalimbali ikiwamo wizi na udokozi uliofanywa na watumishi katika maduhuli na fedha taslimu kabla ya kuwasilishwa benki kwa mujibu wa sheria.

Azimio hilo la Serikali liliwasilishwa bungeni mjini hapa na Naibu Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba ambaye alisema madeni, hasara na upotevu wa mali na fedha ulitokea katika kipindi kinachoishia Juni 30, mwaka 2011.

Alisema hasara na upotevu huo unajumuisha miaka michache ya 1990 na mwingine ukiwa ni kuanzia Julai 2001 hadi Juni mwaka 2011.

Nchemba alisema upotevu huo umefanyiwa uchambuzi na Idara ya Mhasibu Mkuu wa Serikali na kuhakikiwa na Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) kwa mujibu wa sheria.

Alitaja hasara na upotevu huo kwa mwaka ulioshia Juni 30, 2011 kuwa ni pamoja na unaohusu fedha taslimu, ambazo ni zaidi ya Sh milioni 150.1 na wa vifaa ya Serikali zaidi ya Sh bilioni 10.1.

HASARA YA SH MILIONI 150.1

Akizungumzia hasara na upotevu unaohusu zaidi ya Sh milioni 150.1, alisema unahusisha zaidi ya Sh milioni 37.5 katika Jeshi la Polisi, Ofisi ya Mkuu wa Polisi Wilaya (OCD) ya Ilala ambazo zilipotea kwa kutoonekana kwenye akaunti ya benki.

Alisema hasara hiyo pia inahusisha zaidi ya Sh milioni 19.1 katika Ofisi ya Askari Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, ambazo nazo zilipotea kwa kutoonekana kwenye akaunti.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles