22.8 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 22, 2024

Contact us: [email protected]

Hans Pluijm aweka ngumu Yanga

hans-van-der-pluijmJENNIFER ULLEMBO-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans Van der Pluijm, ameuwekea ngumu uongozi wa klabu hiyo ambao unamtaja kuwa Mkurugenzi wa Ufundi, licha ya mazungumzo kati ya pande hizo mbili kuendelea.

Uongozi wa klabu hiyo umependekeza Pluijm kuchukua nafasi hiyo, baada kocha mpya George Lwandamina, kukabidhiwa majukumu kukinoa kikosi hicho.

Habari za kuaminika ndani ya Yanga zinasema, licha ya kocha huyo Mholanzi kuweka ngumu, mazungumzo bado yanaendelea kumshawishi akubali.

Mpasha habari huyo alisema imekuwa ni jambo gumu uongozi kumshawishi Pluijm ambaye ameonyesha nia yake ya kuondoka.

“Mazungumzo yanaendelea na hakuna mwafaka ulioweza kufikiwa hadi sasa, hivyo ni vigumu kusema kuwa Pluijm atakuwa Mkurugenzi wa bechi la ufundi.

“Pluijm ameweza kuisaidia sana timu, ndio maana uongozi unaona kuliko aondoke ni bora akapewa majukumu mengine.

“Unajua mafahari wawili kufanya kazi sehemu moja mara nyingi ni jambo gumu, hasa ukizingatia kuwa Pluijm ana kiwango kizuri cha kuwa kocha na kufanya kazi sehemu yoyote,” kilisema chanzo hicho.

Chanzo hicho kilieleza kuwa kiwango cha Pluijm kinaweza kumpa nafasi ya kufundisha timu yoyote nchini au nje ya nchi.

Pluijm wakati wowote anatarajiwa kukabidhi majukumu yake kwa Mzambia Lwandamina, ambapo tayari kocha  huyo aliyekuwa akiinoa timu ya Zesco yupo nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles