27 C
Dar es Salaam
Sunday, November 17, 2024

Contact us: [email protected]

Halotel yatia mkono Uongozi wa mtaa wa Bwawani kupitia ufadhili wa Iftar

Na Imani, Nathaniel, Mtanzania Digital

Kampuni ya mawasiliano ya Halotel, inayoendelea kuwa mstari wa mbele katika kuleta maendeleo kwa jamii, imejitolea kudhamini tukio la Iftar kwa uongozi wa mtaa wa Bwawani na jamii ya watu wa Makumbusho jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana Naibu Mkurugenzi wa Fedha Halotel, Najib Ferej amesema tukio hilo la Iftar linalenga kuileta pamoja jamii katika kipindi hiki cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.Halotel inaamini katika umoja na mshikamano kama kauli mbiu ya kampuni inavosema ‘Pamoja kwa Ubora’ na tumeona ni muhimu kusaidia juhudi za serikali kuleta watu pamoja na leo tupo tena Makumbusho katika kukuza uhusiano mzuri wa jamii zinazotuzunguka.

Katika mwezi huu Mtukufu wa Ramadhani, Halotel kwa ushirikiano na Serikali tunajivunia kuandaa iftar kwa ajili ya Jamii yetu, hii ni ishara ya Umoja wetu, mshikamano na undugu unaotuunganisha sote. Ni wakati wa kushiriki, kusadiana na kuimarisha mahusiano yetu katika jamii.

“Kupitia udhamini huu, tunawawezesha uongozi wa mtaa wa Makumbusho kufanya tukio la Iftar kuwa la kipekee na la kumbukumbu kwa wakazi wa Makumbusho na wafanyabiashara wadogowadogo wanaozunguka eneo hili. Halotel inatambua umuhimu wa kujenga jumuiya zenye upendo na tunaamini kuwa tukio hili litakuwa fursa nzuri ya kuimarisha mahusiano ya kijamii na kukuza utamaduni,” amesema Ferej.

Ameongeza kuwa Halotel haitoishia hapo katika kuweka mkono katika jamii,na kwamba itaendelea kuweka nguvu katika kukuza umoja na mshikamano katika jamii na  kuboresha huduma zake ambazo zinarahisisha mawasiliano mijini na kijijini.

Upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Bwawani, Ismail Mwenda ameishukuru kampuni ya Halotel Tanzania kwa kuonesha nia ya kuunganisha watu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.

“Hii ni chachu katika jamii kampuni inapoamua kuunganisha watu katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani, inaonesha upendo na mshikamano kati ya watu wa Makumbusho na jamii kiujumla,” amesema Mwenda.

Halotel akiwa ni mtoa huduma wa mawasiliano Tanzania, akitoa huduma mbalimbali za mawasiliano na akiendelea kukidhi mahitaji ya wateja wao. Kwa kuzingatia utoaji huduma bora na uaminifu Halotel inaendelea kutoa huduma bora na kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya mawasiliano na jamii kiujumla.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles