Mwandishi Wetu-Dar es Salaam
KATIKA muendelezo wa kutoa huduma bora za kifedha nchini, Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel kupitia huduma zake za kifedha za HaloPesa, kufanya Gawio kwa wateja wake.
Hatua hiyo ni ya kwanza kwa HaloPesa kutoa gawio kiasi cha Sh bilioni moja kwa wateja wake zaidi ya milioni 1.9 ambao ni pamoja na wateja binafsi, mawakala na washirika wake mbalimbali wanatumia huduma za HaloPesa.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa kitengo cha biashara cha Halopesa, Magesa Wandwi amesema wateja wao Watapita Gawio hilo kupitia akaunti zao za Halopesa.
“Wateja watapata sehemu ya Gawio hili linalotokana na faida iliyozalishwa kutoka katika akaunti za HalotePesa Trust zilizoko katika mabenki mbalimbali nchini kati ya Kktoba 2016 na Desemba 2018, “amesema Wandwi
Amesema kuwa faida hiyo ni haki ya wateja na hivyo HaloPesa tunashauku na furaha kubwa ya kuwalipa wateja wetu gawio hilo kwa mujibu wa sheria ,kanuni na miongozo mbalimbali toka Benki Kuu ya Tanzania (BoT) .
Gawio hilo ni la kwanza kwa wateja wetu, na litatolewa ndani ya mwezi mmoja toka sasa, kiasi cha gawio ambacho mteja wa Halopesa atakipata anaweza kutumia atakavyo ikiwa ni pamoja na kutoa au kufanya miamala mbalimbali.
Tunapenda kuwasihi wateja wetu kuwa Halotel tunaendelea na tutaendelea kutoa huduma bora zenye gharama nafuu nchi nzima na waendelee kutumia huduma zetu za HaloPesa.