33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Jeshi la Magereza Iringa kutatua changamoto ya viwanja vya michezo

RAYMOND MINJA IRINGA

Jeshi la magereza mkoani Iringa linatarajia kujenga uwanja mkubwa na wa kisasa ili kutatua changamoto ya upungufu wa viwanja vya mazoezi na michezo mbalimbali ikiwamo ligi ya soka Tanzania bara.

Ujenzi wa uwanja huo utajumuisha uwanja wa mpira wa kikapu, volibo na uwanja wakuruka kamba  ambapo kwa awamu ya kwanza utagarimu Sh. miloni 44.

Akizungumza na Mtanzania Mkuu wa Magereza Mkoa wa Iringa, ASP Eduthi Mbogo amesema matayarisho ya ujenzi wa uwanja huo  yameshaanza kwa kutumia nguvu kazi waliyonayo kutoka gerezani.

Mbogo amesema uwanja huo ni moja ya kitega uchumi kwani matamasha mbalimbali yatafanyika hapo na msimu wa ligi  kuu utakapoanza timu mbalimbali zitakwenda  kuweka kambi na wao kuingiza kipato kitakachowasaidia kuendesha shunguli mbali mbali za magereza.

“Ujenzi wa uwanja huu wa kisasa pamoja na ujenzi wa sehemu ya kupumzikia watu haya ni maelekeo kutoka kwa Kamishina Mkuu wa Magereza Tanzania, Suleman Mzee kuwa jeshi la magereza linatakiwa kujitegemea kwa kila kitu hivyo tumeamua kujenga miradi mbalimbali huu ukiwa mmoja wapo ili tupate fedha tutakazotumia kununulia wafungwa wetu chakula na vitu vingine,” amesema Mbogo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles