26 C
Dar es Salaam
Friday, November 15, 2024

Contact us: [email protected]

Halopesa kugawa bilioni moja kwa wateja wake

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Kampuni ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Halotel kupitia huduma zake za kifedha za HaloPesa imepanga kutoa gawio la Sh bilioni moja kwa wateja wake.

Hii ni mara ya kwanza kwa HaloPesa kutoa gawio la kiasi hicho cha fedha kwa wateja  wake zaidi ya 1.9M  ambao ni pamoja na wateja binafsi, mawakala na washirika wake mbalimbali wanaotumia huduma za HaloPesa.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Mkuu wa kitengo cha biashara cha Halopesa, Magesa Wandwi amesema wateja wao watapata gawio hilo kupitia akaunti zao za Halopesa.

“Wateja watapata sehemu ya gawio hili linalotokana na faida iliyozalishwa kutoka katika akaunti za HalotePesa Trust zilizoko katika benki mbalimbali nchini kati ya Oktoba na Desemba mwaka huu,” amesema Wandwi.

Amesema faida hiyo ni haki ya wateja na hivyo HaloPesa hivyo wana shauku na furaha kubwa ya kuwalipa wateja wetu gawio hilo kwa mujibu wa sheria, kanuni na miongozo mbalimbali toka Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

“Gawio hilo ni la kwanza kwa wateja wetu, na litatolewa ndani ya mwezi mmoja toka sasa, kiasi cha gawio ambacho mteja wa Halopesa atakipata anaweza kutumia atakavyo ikiwa ni pamoja na kutoa au kufanya miamala mbalimbali,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles