31.2 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Uingereza yaruhusu matumizi ya dawa virusi ya remdesivir

 LONDON, UINGEREZA

TIBA ambayo inaonekana kupunguza muda wa kupona mgonjwa anapopata virusi vya ugonjwa wa corona, imeanza kupatikana katika hospitali za Uingereza.

Dawa ya Remdesivir ina kabiliana na virusi ambayo awali ilikuwa imetengenezwa kutibu viusi vya ugonjwa wa ebola.

Wadhibiti nchini Uingereza, wanasema kuna ushahidi wa kutosha wa kuidhinisha matumizi ya dawa hiyo kwa wagonjwa walio hospitali.

Marekani na Japani pia nazo tayari zimeshafanya maandalizi ya kupata dawa hiyo mapema kabla ya kufikiwa kwa makubaliano ya kibiashara juu ya dawa hiyo.

Kwa sasa dawa inafanyiwa majaribio kote duniani, ikiwemo Uingereza.Takwimu za awali zinaonesha, dawa hiyo ina uwezo wa kupunguza siku za kupona hadi nne.

Bado haijafahamika kampuni ya dawa ya Gilead Sciences, ina dawa hizo kiasi gani kwa ajili ya wagonjwa wa Uingereza. Waziri anayesimamia masuala ya uvumbuzi, Lord Bethell amesema: “Dawa hii inaonesha matokeo mazuri. Tunapoangazia kipindi hiki ambacho kimekuwa cha kipekee, tunatakiwa kuwa mstari wa mbele kwa maendeleo ya tiba, na kuhakikisha usalama wa wagonjwa unasalia kuwa kipaumbele.

“Yaliyotokea hivi karibuni, ushauri wa wataalamu wa kisayansi unazingatiwa katika maamuzi yote yanayofanyika,tutaendelea kufuatiliana mafanikio ya dawa ya remdesivir katika majaribio yanayofanywa kote duniani kuhakikisha matokeo bora kwa wagonjwa wa Uingereza”

Dk.Stephen Griffin kutoka chuo kikuu cha Leeds Medical School, amesema kuwa hii ndo dawa ambayo hadi kufikia sasa imeonesha matumaini zaidi katika magonjwa ya kuambukiza ya virusi.Alisema wagonjwa waliougua sana ndio watakaoewa kipaumbele. “Ikiwa hii ndio dawa pekee ambayo inaonesha kuwa na matokeo mazuri, hai maanishi kwamba watu watarajie miujiza ya siku moja.

“Badala yake tunaweza kuwa na matuamini ya wagonjwa wengi kupona na kupungua kwa vifo vya watoto, tukiwa na matumaini kwamba itakuwa na manufaa kwa wagonjwa wengi zaidi”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles