24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, April 17, 2024

Contact us: [email protected]

Mtoto wa mwezi mmoja augua ugonjwa wa corona

 SAMMY WAWERU na CHARLES WASONGA

MTOTO mwenye umri wa mwezi mmoja, ni miongoni mwa wagonjwa waliothibitishwa na Naibu Waziri wa Afya, Dk. Rashid Aman alipotoa takwimu za idadi ya maambukizi mapya ya Covid-19 katika kipindi cha saa 24 ambazo zimepita.

Visa vya Covid-19, sasa ni 1,888 baada ya kuthibitishwa vingine 143 baada ya wizara kufanyia vipimo sampuli za watu 2,959 na mgonjwa mwenye umri wa juu ana umri wa miaka 88.

“Wagonjwa wote ni Wakenya ambapo 110, ni wa jinsia ya kiume na 33 ni wa jinsia ya kike,” Dk. Aman.

Dk.Aman alisema mgonjwa mmoja amefariki dunia, akiwa na umri wa miaka 53 ambapo idadi ya walioaga dunia nchini kutokana na Covid-19 sasa ikifika watu 63.

Kaunti ya Nairobi na Mombasa, zingali zinaongoza katika maambukizi, Nairobi ikithibitisha maambukizi mapya 88 na Mombasa 25.

Kaunti ya Kericho, imekuwa ya hivi punde kuthibitisha maambukizi ya ugonjwa huu, baada ya kisa kimoja kuthibitishwa kutoka huko, idadi jumla ya kaunti zilizoathirika sasa ni 33.

Dk.Aman alitangaza watu 26 wameruhusiwa kuondoka hospitalini, baada ya kupona, idadi jumla ya waliopona Covid-19 sasa ikifika 464.

“Kutokana na visa hivi vipya, sasa idadi jumla ya visa vya maambukizi nchini imetimu 1888,”alisema.

Alisema miji ya Nairobi na Mombasa, inakabiliwa na visa vingi vya maambukizi. Katika mtazampo wa kaunti, Nairobi ina visa vipya 86, Mombasa (25), Uasin Gishu (11), Kiambu (6), Busia (3), Kwale (3), Migori (3), Kajiado (1), Kisii (1), Garissa (1), Isiolo (1), Makueni (1) na Kericho (1).

Katika kaunti ya Nairobi, Makadara inaongoza kwa visa 45, Kibra (21), Embakasi Kusini (6), Kasarani (5), Ruaraka (3), Westlands (2), Embakasi Magharibi (2), Langata (1) Starehe (1).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles