23.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Halmashauri ya Meru yapata elimu ya kukabiliana na maafa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa, Luteni Kanali Selestine Masalamado amesema elimu ya usimamizi wa Maafa itaendelea kutolewa kwa wananchi  kwa maeneo yanaoathirika kwa matukio ya tofauti tofauti ya maafa.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya akizungumza na washiriki wa mafunzo ya elimu ya kukabiliana na maafa yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.

“Tunatoa elimu kwa wananchi ili kujenga uelewa wanamna ya kukabiliana na maafa, kwa kueleza dhana ya maafa, kueleza maana ya majanga ikiwa pamoja na kuangalia mzingo wa maafa kwa ujumla,” amesema Masalamado.

Hayo yamesemwa jana na Luteni Kanali Selestine Masalamado Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Menejimenti ya Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kwa kushirikiana na Shirika la kimataifa la Uhamiaji (IOM) katika kikao cha mafunzo ya Udhibiti wa Maafa kwa jamii yaliyofanyika Halmashauri ya Wilaya ya Meru na kuhusisha wananchi wa kata ya Mbuguni na Shambaray Bruka.

 “Washiriki wameelewa mfumo mzima wa Kudhibiti Maafa kwa kuanzia ngazi ya taifa hadi kufikia ngazi ya Kijiji,” amesema Luteni Kanali Masalamado.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru Mwl. Zainabu Makwinya ameshukuru Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) kwa kufanya mafunzo hayo Halmashauri ya Wilaya ya Meru.

“Tunashukuru kwa kutuongezea wataalamu wa maafa kupitia mafunzo yaliyoyotolewa ili kutusaidia namna ya kukabiliana na Maafa,” Zainabu.

Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya menejimenti ya Maafa, Luteni Kanali Selestine Masalamado akiwa na washiriki walio katika makundi wakati wa mafunzo ya elimu ya kukabiliana na Maafa yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.

Mwl. Makwinya amefanunua kata ya Shambaray Bruka na Mbuguni yamekuwa yakiathirika na mafuriko na ukame.

Ametoa wito kwa washiriki kutoa elimu kwa wananchi ili kuongeza maarifa kwa  kusaidia maeneo mengine yanayoyoathirika na maafa.

Naye Mshiriki kutoka kata ya Mbuguni, Fanael Kaaya amesema mafunzo ya kukabiliana na maafa waliyopata imesaidia kuchukua tahadhari ya kujikinga na maafa kabla hajatokea ikiwemo kutengeneza matuta ya kuzuia maji kwenye maeneo yanayoathirika na mafuriko na pamoja kufukua mifereji iliyoziba pamoja na mito ili mafuriko ya maji yanapokuja yaweze kupita.

Dk. Baltazari Leba Mratibu wa Idara ya menejimenti ya maafa Ofisi ya waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu) akiwa na washiriki wakati mafunzo ya elimu ya kukabiliana na maafa yaliyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meru.
- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles