London, Uingereza
IMEFICHUKA kuwa chanzo cha straika wa Borussia Dortmund, Erling Haland, kutotua Chelsea ni wakala wa mchezaji huyo wa kimataifa wa Norway.
Kwamba wakala huyo, Mino Raiola, alitaka alipwe mkwanja mrefu ili akubali Haaland kujiunga na miamba hiyo ya jijini London.
Kiasi cha fedha alichokitaka Raiola, pamoja na ada ya usajili ambayo Dortmund wangepokea ingewafanya Chelsea watumie Pauni milioni 275 kuinasa saini ya Haland.
Baada ya kushindwa kumudu gharama hizo, ndipo mabosi wa Chelsea walipomgeukia straika wao wa zamani aliyekuwa akikipiga Inter Milan, Romelu Lukaku.