28.4 C
Dar es Salaam
Thursday, February 22, 2024

Contact us: [email protected]

Guterres ato wito wa uchaguzi huru Uganda

New York, Marekani

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametoa wito wa mchakato wa uchaguzi ulio jumuishi, wa amani, na wa wazi nchini Uganda.

Gutarres ameeleza wasiwasi wake kutokana na ripoti za vurugu na mvutano mkali katika baadhi ya maeneo nchini Uganda, na kuwataka wanasiasa wote na wafuasi wao kujizuia na matumizi ya kauli za chuki, vitisho na mabavu.

Aidha, amerejea ahadi ya Umoja wa Mataifa ya kuunga mkono juhudi za nchi hiyo za kuboresha maendeleo endelevu na kujenga siku za baadaye zenye ustawi.

Uchaguzi Mkuu wa rais na wabunge unafanyika leo nchini Uganda, huku rais wa sasa wa nchi hiyo, Yoweri Museveni, aliyekuwa madarakani kwa muda mrefu, akigombea tena kuendelea na wadhifa huo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
583,000SubscribersSubscribe

Latest Articles