24.9 C
Dar es Salaam
Sunday, April 21, 2024

Contact us: [email protected]

Guninita kulishtaki gazeti MCT

gununitaNA KOKU DAVID, DAR ES SALAAM
MWENYEKITI Mstaafu wa Chama cha Mapinduzi (CCM)MKoa wa Dar es Salaam, John Guninita, amesema anakusudia kulishitaki gazeti la kila wiki la Sauti Huru kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) kwa madai ya kuandika habari za uchonganishi dhidi yake.
Katika taarifa yake, kada huyo wa CCM alidai kuwa gazeti hilo toleo Namba 331 la Machi 12 mwaka huu liliandika habari za fitina, ugombanishi na uchochezi.
Guninita alisema habari hiyo iliyokuwa na kichwa cha habari kisemacho, ‘Hivi Lowasa ni rafiki wa kweli na wa dhati?’ haikuwa na ukweli wowote.
“Sijasema wala kuandika E-mail yoyote kama anavyodai mhariri kwani namheshimu sana Lowasa na natambua kuwa ni kiongozi mahiri na mchapa kazi kama alivyoweza kuweka kumbukumbu mbalimbali za ujenzi wa Taifa hili,” alisema.
Katika taarifa hiyo alieleza kuwa yaliyoandikwa kwenye makala hiyo siyo yake na kwamba yameandikwa na mhariri kwa masilahi ya kificho cha gazeti hilo.
“Ili haki itendeke nimeamua kulipeleka suala hilo MCT wachunguze ukiukaji wa maadili ya uandishi,”ilisema sehemu ya taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles