24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, January 9, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Griezmann: Barcelona pagumu

BARCELONA, HISPANIA

MSHAMBULIAJI wa timu ya Barcelona, Antoine Griezmann, ameweka wazi kuwa, kucheza soka ndani ya kikosi hicho sio kazi rahisi, lakini anaamini atapambana kuhakikisha anapigania nafasi kwenye kikosi cha kwanza.

Staa huyo amejiunga na Barcelona wakati wa uhamisho wa kiangazi mwaka huu akitokea Atletico Madrid, lakini tangu kujiunga kwake bado hajaonesha kiwango ambacho wengi walitarajia kikuona.

Hali hiyo inatokana na mabadiliko ya namba akiwa Atletico Madrid na Barcelona ni tofauti, hata hivyo kuna ushindani mkubwa wa namba.

Katika michezo 11 aliyocheza msimu huu mchezaji huyo amefanikiwa kupachika manne ya Ligi Kuu nchini Hispania huku akitoa pasi tatu za mwisho, hivyo mashabiki wamedai mchezaji huyo bado yupo chini ya kiwango.

Mashabiki waliamini ujio wa mchezaji huyo utakuwa na mchango mkubwa wa mafanikio ya timu huku akiweza kuziba nafasi ya aliyekuwa nyota wa timu hiyo Neymar Jr ambaye kwa sasa anakipiga katika klabu ya PSG.

Kocha wa Barcelona, Ernesto Valverde, aliweka wazi kuwa kiwango cha Griezmann kitakuja kubadilika endapo atakubali kufuata misingi ya timu hiyo, lakini mkurugenzi wa michezo wa timu hiyo Eric Abidal amedai mchezaji huyo bado yupo chini ya kiwango.

“Barcelona sio sehemu rahisi kucheza mpira, hii ni timu mpya kwangu, nimetoka kwenye timu nyingine ambayo niliizoea, nimekutana na mbinu mpya, nafasi nyingine ya kucheza, lakini haijalishi, huu ndio muda sahihi wa kupambana kwa ajili ya kupigania timu na kupigania namba yangu kikosini.

“Ninajivunia maamuzi yangu ya kuwa hapa kwa sasa, ninaamini kila kitu kitakuwa sawa, lengo langu kwa sasa ni kuhakikisha ninakuwa mchezaji muhimu ndani ya kikosi, kucheza dakika nyingi, kufunga mabao mengi, kutoa pasi na kuifanya timu inafuzu michuano ya Ligi ya Mabingwa,” alisema mchezaji huyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles