22.5 C
Dar es Salaam
Sunday, July 21, 2024

Contact us: [email protected]

Global link kusaidia Watanzania waliokuwa wanasoma Sudan

Na Nora Damian, Mtanzania Digital

Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Link) imeanzisha dawati maalumu kusaidia Watanzania waliokuwa wanasoma Sudan ili waweze kupata vyuo katika mataifa mengine.

Aprili mwaka huu baadhi ya Watanzania waliokuwa wanasoma nchini humo walilazimika kurudi nchini kutokana na mapigano yanayoendelea nchini humo.

Akizungumza Dar es Salaam na waandishi wa habari Julai 18,2023 kwenye maonesho ya vyuo vikuu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Uwakala wa Vyuo Vikuu Nje ya Nchi (Global Link), Abdulmalik Mollel, amesema vyuo vikuu 16 kutoka katika nchi nane vinashiriki kwenye maonesho hayo.

“Tumeanzisha dawati maalumu kusaidia Watanzania waliokuwa wanasoma Sudan, vyuo vikuu vya ndani vyenye uwezo wa kuwachukua viwachukue, na kwa wale wanaotaka kuendelea kusoma nje waje tutawasaidia watapata vyuo kwa gharama nafuu na watafanya udahili hapa.

“Wasiendelee kupoteza, hatujui machafuko yatakwisha lini, mwanafunzi aliyekwama ametoka Sudan na anatamani kuendelea na masomo nje ya nchi njoo tutakusaidia,” amesema Mollel.

Pia amevitaka vyuo vikuu kuchangamkia fursa ya ushirikiano na vyuo vikuu vya nje na kwamba viko vyuo vikuu 16 kutoka katika nchi nane ambavyo vimeshiriki kwenye maonesho hayo.

“Jukumu lingine kubwa tutakalofanya kwenye maonesho haya ni kuvisimamia vyuo vikuu vya ndani na vya nje ili visaini makubaliano yenye tija,” amesema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles