24.4 C
Dar es Salaam
Thursday, October 31, 2024

Contact us: [email protected]

Giroud akiri kufunga kwa mkono

Olivier Giroud says Arsenal have the players and team spirit to be serious contenders next season.LONDON, ENGLAND

MSHAMBULIAJI wa Arsenal, Olivier Giroud, amekiri kuwa mkono wake ulisaidia kupatikana kwa bao la kwanza la timu yake katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich juzi usiku kwenye Uwanja wa Emirates, England.

Katika mchezo huo wa raundi ya tatu wa Kundi F, Arsenal walishinda mabao 2-0, lingine likiwekwa kimiani dakika za majeruhi na kiungo Mjerumani, Mesut Ozil.

Mfaransa huyo aliyeingia uwanjani dakika 13 kabla ya mchezo kumalizika, alifunga bao dakika tatu baadaye ambapo mpira uliozaa bao ulionekana kutua kwenye pua yake na kumparaza mkononi kabla ya kutinga nyavuni.

Akilielezea bao hilo, Giroud alisema kuwa mkono wake ulimsaidia mno kufunga akifika mbali zaidi kwa kuliita ‘Bao la Mkono wa Mungu’.

Giroud, aliyenufaika na kosa lililofanywa na kipa wa Bayern, Manuel Neuer, alisema: “Kwa mshambuliaji huwa inakuwa hivyo katika mchakato mzima wa kutafuta bao na ninafahamu hilo. Huwezi kujitilia shaka.

“Lilikuwa ni bao la ubora wa hali ya juu na nilihitaji msaada wa mkono kupata bahati ile na usiku wa leo (juzi) ilikuwa hivyo. Sasa tunaweza kuangalia mbele.

“Ilikuwa vizuri kushinda mechi hii kwasababu inamaanisha bado tupo kwenye mstari wa kuelekea hatua ya 16 bora, lakini tutahitaji kuzifunga Olympiakos na Zagreb.”

Baada ya mchezo huo, kocha Arsene Wenger alisema: “Nina washambuliaji wawili wa kiwango cha juu na ninawatumia wote kwa pamoja. Kwa siku za karibuni ni Walcott, lakini nina mambo mengi ninayoyapata kutoka kwa Giroud na wote wawili watacheza.”

Kocha huyo ambaye vijana wake wataikaribisha Everton katika mchezo wa Ligi Kuu England Jumamosi, aliongeza: “Tunahitaji matokeo dhidi ya Bayern katika mchezo wetu ujao lakini ngoja tuelekeze akili zetu kwa Everton.”

Kipa wa Arsenal, Petr Cech, alicheza vizuri mno juzi akiokoa hatari kadhaa kutoka kwa washambuliaji wa Bayern kama Robert Lewandowski, Thiago

Alcantara, Douglas Costa na Thomas Muller.

Juu ya kipa huyo, Wenger alisema: “Petr Cech ndiye aliyekuwa shujaa wetu. Alikuwa ni mwerevu mno, kila alichofanya kilikuwa cha kiwango cha juu. Kulikuwa na makipa wawili wa kiwango cha dunia usiku wa leo (juzi).”

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles