MSANII chipukizi wa muziki wa kizazi kipya, Amina Hussein ‘Mina’, ametamba kumpoteza Rubby kwenye ramani ya muziki kutokana na uwezo mkubwa alionao.
Mina hivi sasa anafanya vizuri mkoani Kilimanjaro na wimbo wake unaoitwa ‘Najiamini’.
“Kwa sasa muziki wangu unasikika na kupendwa zaidi mikoani, kikubwa ambacho nitakifanya ili nitimize azma yangu ni kujikita katika utunzi kitu ambacho Rubby hawezi pamoja na kutengeneza ‘network’ kubwa ndani na nje ya Tanzania,” alisema Mina kwa kujinadi.