29.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 18, 2024

Contact us: [email protected]

GGM yafadhili madawati 10,000 Geita

Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Terry Mulpeter, akishikana mkono na mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mseto akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hermani Kapufi na wakati wa makabidhiano ya madawati juzi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), Terry Mulpeter, akishikana mkono na mwanafunzi wa Shule ya Msingi Mseto akiwa na Mkuu wa Wilaya ya Geita, Hermani Kapufi na wakati wa
makabidhiano ya madawati juzi.

Na MWANDISHI WETU – GEITA

MGODI wa Dhahabu wa Geita (GGM), umetumia Sh milioni  750 kutengeneza madawati 10,000 ambayo yamekabidhiwa kwa uongozi wa Mkoa wa Geita ili yagawanywe katika wilaya tano za mkoa huo.

Akipokea madawati hayo kwa niaba ya mkuu wa mkoa jana, Mkuu wa Wilaya ya Geita, Herman Kapufi, alisema msaada huo utasaidia kumaliza tatizo kubwa la uhaba wa madawati.

“Tunapenda kushukuru mchango huu wa madawati, pia natambua jitihada nyingine za maendeleo zinazofanywa na mgodi wa GGM, ni jambo jema kuongeza misaada hii, mkoa wetu utaendelea kufanya vyema katika sekta ya elimu kwa kuwa ufaulu wa wanafunzi wa shule za msingi umeanza kuimarika,” alisema.

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Geita, Modest Apolinary, alisema mchango huo ni muhimu katika kuboresha elimu kwenye halmashauri hizo.

“Halmashauri ya Mji wa Geita ilikuwa na upungufu wa madawati 11,773, wakati yaliyopo ni 13,609, huku mahitaji yakiwa ni 25,190. Wilaya ya Geita ilikuwa na upungufu wa madawati 22,066, yaliyopo ni 33,514 na mahitaji ni 55,580.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mtendaji wa GGM, Terry Mulpeter, alisema mgodi huo kama jirani mwema, umeguswa na upungufu wa madawati mkoani Geita na ndiyo sababu umeamua kuunga mkono jitihada za Serikali.

Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Mseto, Grace Ndimuhele, alisema shule yake ina wanafunzi 1,266, lakini ina madawati 133, hivyo mchango wa GGM umekuwa mkombozi kwao.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles