23.6 C
Dar es Salaam
Saturday, April 27, 2024

Contact us: [email protected]

GESI, MAFUTA VYAZUA JAMBO MTWARA

Na Florence Sanawa, Mtwara

Ugunduzi wa nishati ya gesi na mafuta mkoani Mtwara, imeibua changamoto ya uhaba wa maeneo ya kufanyia kazi kwa wajasiriamali wadogo hali inayotokana na ongezeko la watu wenye mahitaji ya nishati hiyo.

Changamoto hiyo imelikumba Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) Mkoa wa Mtwara, ambalo linakabiliwa na uhaba wa majengo ya kufanyia uzalishaji wajasiriamali wadogo licha ya kuwa na eneo lenye ukubwa zaidi ya hekari nane.

Meneja wa SIDO mkoani Mtwara, Joel Chidabwa amesema  mbali na mahitaji hayo kuongezeka lakini mkoa unakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo ukosefu wa hati miliki  kwenye eneo la Mtaa wa Viwanda SIDO hali inayosababisha eneo hilo kutoendelezwa.

“Uchache wa majengo kwenye eneo hilo, inasababisha wanaotaka kuanzisha kukosa majengo ya kufanyia shughuli zao.

“Kwa muda mrefu tumekuwa tukitafuta na kusambaza teknolojia mbalimbali kwa wajasiriamali Mkoa wa Mtwara ili kuwaongezea ujuzi zaidi ikiwamo usindikaji wa chumvi, urinaji wa asali, uchongaji na uchomeleaji wa vyuma zaidi ya vitu 236 vilifundishwa

“Tunazo zaidi ya hekari ziko wazi hazijaendelezwa na zinaweza kutumiwa kwa ajili ya viwanda kwa kujenga majengo ambayo yanaweza kutumika kwa shughuli mbalimbali za viwanda,” amesema Chidabwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles