23.8 C
Dar es Salaam
Sunday, October 13, 2024

Contact us: [email protected]

MAANDALIZI WIKI YA MLIPAKODI YAKAMILIKA, KUANZA KESHO NCHI NZIMA

Na Veronica Kazimoto, Dar es Salaam

Wafanyabiashara na wananchi kwa ujumla, wamehimizwa  kujitokeza kwa wingi katika vituo vilivyopangwa rasmi kwa ajili ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi itakayoanza kesho Machi 5-9, mwaka huu nchi nzima.

Akizungumza leo Jumapili Machi 4, jijini Dar es Salaam Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi, katika Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Richard Kayombo amesema maandalizi yamekamilika katika vituo vyote hivyo wananchi watumie fursa hii kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu kodi.

“Maandalizi ya Wiki ya Elimu kwa Mlipakodi yamekamilika kwa kiasi kikubwa, niwaombe tu wafanyabiashara na wananchi wote wajitokeze kwa wingi katika vituo vilivyotengwa rasmi katika kila mkoa nchi nzima kwa ajili ya kupata uelewa zaidi juu ya masuala ya kodi, kutoa malalamiko, mirejesho, changamoto na maoni mbalimbali,” amesema Kayombo.

Pamoja na mambo mengine, Kayombo ameweka wazi kuwa  katika wiki hiyo mada mbalimbali zitafundishwa kama vile ulipaji wa Kodi ya Majengo kwa njia ya kieletroniki, Mkataba wa Huduma kwa Mlipakodi ambao umeainisha haki na wajibu wa mlipakodi na viwango vya huduma wanavyopaswa kupata kutoka TRA pamoja na umuhimu wa kutoa na kudai risiti ikiwa ni pamoja na kikagua kabla ya kuondoka nayo.

“Watalaam wetu wamejipanga vizuri kutoa elimu katika kila mkoa kwenye wiki hii ya elimu kwa mlipakodi. Mada mbalimbali zitafundishwa ikiwa ni pamoja na kuwakumbusha wananchi kulipa kodi inavyostahili ndani ya muda utaotakiwa,” amesema Kayombo.

Wiki ya elimu kwa mlipakodi kwa sasa, itakuwa inafanyika kila baada ya miezi mitatu ikiwa na lengo la kuelimisha, kusikiliza malalamiko, changamoto, kupokea mrejesho pamoja na maoni mbalimbali kutoka kwa walipakodi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles