26.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Gazidis: Arsenal itakuwa noma

Ivan Gazidis
Ivan Gazidis

LONDON, ENGLAND

MKURUGENZI Mtendaji wa klabu ya Arsenal, Ivan Gazidis amesema kwamba klabu hiyo itatumia fedha kama itaona umuhimu wa kufanya hivyo huku akiamini kikosi cha timu hiyo kwa sasa kipo vizuri kushinda Ubingwa wa Ligi kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2004.

Gunners ilimaliza msimu uliopita ikiwa nafasi ya pili nyuma ya bingwa wa msimu huo, Leicester City ingawa Arsenal ilikuwa kinara mwanzoni mwa msimu.

Kauli hiyo ya  Gazidis ilimaanisha kwamba Arsene Wenger atakuwa akishindana kwa karibu na Chelsea, Manchester United na Manchester City.

Lakini Arsenal wanaamini kwamba wana fedha za kutosha licha ya msimu uliopita kuwakasirisha mashabiki wa timu hiyo kutosajili licha ya kuwa na akiba ya pauni milioni 100.

Katika msimu uliopita Wenger alifanikiwa kusajili wachezaji wawili tu katika kikosi chake, kipa Petr Cech akitokea Chelsea na kiungo  Mohamed Elneny aliyetokea Basel.

Katika maandalizi tayari kocha huyo amepata saini ya Mswitzerland Granit Xhaka.

Lakini Gazidis aliwaonya mashabiki wa timu hiyo wasitarajie matumizi ya fedha nyingi katika usajili wa wachezaji kama ambavyo wapinzani wao wanavyofanya.

“Hatua hii inatufanya kuwa na nguvu si kwa matumizi makubwa ya fedha ni kwa namna ya kutumia fedha katika matumizi muhimu.

“Tunajivunia  kutumia dira sahihi yenye  thamani ndani ya klabu ambapo tunaweza kununua wachezaji na ikawa fahari kwa mashabiki,” alisema Gazidis wakati akihojiwa na mtandao wa ESPN.

Arsenal walitarajia kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Lens ya Ufaransa kabla ya kutua jijini Marekani kwa ajili ya mechi mbili za kirafiki.

Gazids alisisitiza kwamba wataendelea kutumia sera yao wakiamini juu ya vipaji chipukizi na kuwa tofauti na klabu nyingine kubwa zinazotumia fedha nyingi kwa ajili ya kuwa na wachezaji mastaa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles