28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

Gazeti Mtanzania kusitishwa kuanzia Jumatatu

Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

KAMPUNI ya New Habari (2006) Ltd, imesema kuanzia Jumatatu ya wiki ijayo itasitisha uzalishaji wa gazeti la MTANZANIA kuanzia Mei,20 hadi Juni 20, mwaka huu kutokana na mabadiliko makubwa ya muundo yanayoendelea.

Taarifa iliyotolewa na uongozi wa kampuni hiyo Dar es Salaam jana, ilisema uamuzi huo umefikiwa baada ya kampuni  kubadili muundo na uendeshaji  na kwamba gazeti hilo sasa litapatikana kwa njia ya digitali kwa kipindi chote hicho.

“Kampuni inautangazia umma na wateja wake kuwa hivi sasa kampuni inabadili muundo wa uendeshaji na uzalishaji, pia kubadili mwelekeo kutoka ‘print’ kwenda digital, hatua hiyo itaendana pia na kupunguza wafanyakazi.

“Ili kuendana na mabadiliko ya biashara, tunapenda kuutangazia umma kuwa kuanzia Jumatatu Mei 20. 2019 gazeti la MTANZANIA halitakuwa likichapishwa kwa kipindi cha mwezi mmoja, hivyo uzalishaji utarajea baada ya mwezi mmoja,”ilisema taarifa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles