32.2 C
Dar es Salaam
Sunday, November 24, 2024

Contact us: [email protected]

Gasco kutumia kamera kubaini bomba la gesi

Faraja Masinde -Dar es salaam

KAMPUNI Tanzu ya Gesi Tanzania (Gasco), imesema inatarajia kutumia kamera za juu(drones) ili kubaini maeneo ya miundombinu ya bomba la gesi asilia yaliyoathiriwa na mvua ili yaweze kufanyiwa matengenezo.

Hayo yalibainishwa mwishoni mwa wiki na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Gasco ambayo ni kampuni tanzu ya Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania(TPDC), Baltazar Mrosso baada ya kutembelea moja ya eneo la bomba hilo lililopo Kinzudi, Kara ya Goba,Dar es Salaam ambalo limeathiriwa na mvua na kusababisha udongo uliokuwa umelifunika kuzolewa na maji.

Alisema wanatarajia  baada ya mvua zinazoendelea kunyesha kuisha, watapita maeneo yote yaliyoathiriwa ili kuyafanyia matengenezo.

“Mpaka sasa yapo maeneo kama sita ambayo tayari tuna taarifa zake yamepata madhara,yote yatarekebishwa kwa utaratibu, kwa yale yaliyoathirika kidogo yatarekebishwa haraka na yaliyoathirika zaidi wakandarasi watatumika kuyatengeneza ili mvua nyingine zikija yasipate madhara.

“Kina maeneo yaliyoathirika ambayo tuna taarifa zake hadi sasa ambayo yako Dar es Salaam, Mkuranga na Mtwara,” alisema Mrosso.

Mrosso alitumia fursa hiyo kuwatoa hofu wananchi wanaoishi jirani na maeneo ambayo mabomba yameharibika kwa kueleza athari zilizotokea hazina madhara kwao kutokana na uimara wa mabomba ynayotumiwa na TPDC.

Aliwakumbusha wananchi wanaozunguka maeneo hayo,hakuna anayeruhusiwa kufanya shughuli yoyote kwenye miundombinu hiyo.

“Niendelee kusisitiza wananchi wote waliopitiwa na miundombinu hii wanatakiwa kuwa walinzi na kutofanya shughuli zozote za kijamii kwenye miundombinu hii, kuna mabomba yanayopitisha gesi yenye mkandamizo wa hali ya juu ambayo ni mabomba ya chuma na yale yanayopitisha gesi yenye mkandamizo wa chini yaliyotengenezwa kwa plastiki hayo yanatumika kusmbaza gesi mjumbani na viwandani.

“Iwapo mwananchi atapiki juu ya bomba hilo la plastiki maana yake ni kwamba moto ukienda chini unaweza kuleta madhara ndiyo maana haturuhusu watu kufanya shughuli na zipo alama kuonyesha mahala mabomba yalikopita,” alisema Mrosso.

Mkuu wa Kitengo cha Ulinzi na Usalama wa Gasco, Roderick Ntabuoyo alisema bombo hilo limepita mikoa ya Mtwara, Lindi, Pwani na Dar es Salaam na katika miundombinu hiyo upo ulinzi unaozuia shughuli zozote kufanyika ikiwa ni pamoja na ufugaji, kilimo na shughuli za ujenzi ukiwamo wa nyumba.

Menyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Kinzudi, Edward Mbwiga alisema wamekuwa wakishirikiana na Gasco na TPDC kwa kutoa taarifa kwao pale kunapokuwa na uharibifu wa miundombinu hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles