32.2 C
Dar es Salaam
Monday, November 25, 2024

Contact us: [email protected]

Gaidi aliyelipua Ubalozi Dar afungwa maisha Marekani

A courtroom sketch shows Khalid al-Fawwaz at the New York federal courtWASHINGTON, Marekani

MSHIRIKA wa aliyekuwa gaidi namba moja duniani, Osama bin Laden, Khaled al-Fawwaz, amehukumiwa kifungo cha maisha jela nchini Marekani.

Khaled al-Fawwaz amehukumiwa kifungo hicho baada ya kukutwa na tuhuma za kujihusisha na mpango wa mashambulizi ya kigaidi yaliyotokea katika Ubalozi wa Marekani nchini Tanzania na Kenya mwaka 1998.

Kwa mujibu wa mtandao wa habari wa AP, hukumu hiyo ilitolewa na Jaji Lewis Kaplan wa Mahakama ya Manhattan, iliyopo mjini New York.
Mashambulizi ya kigaidi ya mwaka 1998 yaliyofanywa katika balozi za Marekani hapa nchini na Kenya yalisababisha vifo vya watu 224, wakiwamo raia wa Marekani.
Kwa upande wake, mwanasheria wa al-Fawwaz aliiomba mahakama impunguzie kifungo mteja wake huyo.
Awali msoma mashitaka wa serikali alidai kuwa al-Fawwaz alikuwa kiongozi wa kundi la kigaidi la Al-Qaeda na alimsaidia Osama katika azimio lake la mwaka 1996 la vita dhidi ya taifa la Marekani.
Alisema kuwa mtuhumiwa pamoja na kikundi chake walidai watafika sehemu zote za Marekani kwa maana ya kufanya mashambulizi katika mataifa mbalimbali yaliko masilahi ya Marekani.
Al- Fawwaz ambaye ni mzaliwa wa Saudi Arabia, alitiwa nguvuni na wanausalama wa Marekani mwaka 2012 nchini Uingereza.
Kikundi cha kigaidi cha Al-Qaeda kinatajwa kuwa na mtandao mkubwa katika mataifa mbalimbali duniani, lakini nguvu yake kwa sasa inaonekana kupungua baada ya kiongozi wa kundi hilo, Osama Bin Laden, kuuawa na makomandoo wa Marekani nchini Pakistani mwaka 2011.
Hata hivyo, nguvu ya kikundi hicho kwa sasa inaonekana kugawanyika na kuzaa vikundi mbalimbali vya kigaidi, kama vile wanamgambo wa Al-Shabaab kwa ukanda wa Afrika Mashariki, Boko Haram nchini Nigeria na Afrika Magharibi kwa ujumla na wapiganaji wa dola ya Kiislamu (IS) ambao kwa sasa wanasumbua eneo la Mashariki ya Kati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles