27.5 C
Dar es Salaam
Thursday, March 28, 2024

Contact us: [email protected]

Filikunjombe sasa amgeukia Mungu

deo-filikunjombeNa Mwandishi Wetu, Ludewa
MBUNGE wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM)amewaomba viongozi wa dini nchini kuendelea kuwaombea viongozi wa serikali wakiwamo wabunge ili wawatumikie wananchi kwa kutanguliza hofu ya Mungu.
Kauli hiyo aliitoa jana wakati wa mazishi ya aliyekuwa mtawa wa Kanisa Katoliki Parokia ya Imiliwaa, marehemu Insetrud Maria.
Alisema viongozi wa dini wamekuwa wakifanya kazi ya kuliombea taifa na watu wake lakini wanasiasa na viongozi wa serikali wamekuwa wakiwatumikia wananchi kimwili hivyo kuna haja ya viongozi wa dini kuendelea kufanya kazi ya kuwaombea viongozi.
“Maandiko matakatifu yanasema; ‘enendeni duniani mkawafanye watu wote kuwa wanafunzi wangu’…chama cha walimu hapa wamesema kuwa Sr.Maria alikuwa mwalimu mzuri hivyo ni wazi alizifanya kazi zote, ya kiroho na kimwili,” alisema.
Kwa kutambua mchango wake alioutoa duniani enzi za uhai wake, mbunge huyo aliahidi kujenga darasa katika shule ya sekondari parokiani hapo kama njia ya kumuenzi zaidi.
Filikunjombe alisema kumbukumbu hiyo itakuwa kielelezo cha mchango wa Sr.Maria katika maendeleo ya Mkoa wa Njombe.
” Sr.Instrud Maria mbali ya kazi yake ya utawa pia alikuwa ni mwalimu na mchango wake katika shughuli zake ni mkubwa hivyo nawaombeni tumuenzi kwa kujenga darasa moja ambalo litaandikwa jina lake kama kumbukumbu ya sasa na baadaye,”alisema Filikunjombe.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles