23.2 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

FILAMU KENYA KUWANIA OSCAR, BONGO MUVI MPO?

NA CHRISTOPHER MSEKENA

FILAMU fupi inayoitwa Watu Wote au All Of Us kutoka nchini Kenya, wiki hii imechaguliwa kuwania tuzo kubwa duniani za Oscar (90th Oscars Annual Academy Awards), zitakazotolewa katika ukumbi wa Dolby, uliopo Los Angeles, California, Marekani, Machi 4, mwaka huu.

Filamu hiyo iliyojipatia mafanikio makubwa ndani na nje ya Kenya, imechaguliwa kuwania tuzo katika kipengele cha Filamu Fupi za Matukio ya Kweli, ambapo itashindana na filamu fupi nyingine nne kutoka kila pande za dunia, kama Dekalb Elementary, The Eleven O’Clock, My Nephew Emmett na The Silent Child.

Watu Wote au All Of Us ni filamu iliyoweza kubeba uhalisi wa tukio la kweli la kigaidi lililofanywa na kundi la Al-shabaab, lililowahi kutokea eneo la Mandera, nchini Kenya, mwaka 2014, huku ikiangazia maudhui ya uadui wa kidini kati ya Wakristo na Waislamu, yaliyojiri kwenye tukio hilo la kigaidi.

Filamu hiyo imekuwa ni filamu pekee kutoka ukanda huu wa Afrika Mashariki kutia mguu kwenye tuzo hizo kubwa duniani, jambo linalotakiwa ligonge kwenye vichwa vya waandaaji wa filamu, hususan wale wa Tanzania.

Hapa kuna mambo kadhaa ambayo wasanii wa filamu na waandaaji wanapaswa kuyazingatia ili kufikia rekodi hii iliyowekwa na wasanii wa Kenya.

Ukiitazama filamu hiyo fupi (Watu Wote/All Of Us), utabaini ni filamu iliyobeba hadithi ya tukio la kweli na kuigizwa na wasanii walioweza kuuvaa uhusika ipasavyo. Waandaaji wa sinema hiyo walilenga kufanya kazi itakayoleta mapinduzi ya kweli.

Ndiyo maana wakakubali kufanya kitu kidogo, walichowekeza nguvu, fedha na maarifa yaliyoleta tija kwa tasnia nzima. Hawakuona haja ya kutengeneza filamu ndefu yenye maudhui yasiyogusa jamii yao.

Wamewekeza kwenye tukio la kweli na kutimiza lengo lao lililozaa faida kwenye kiwanda kizima cha filamu Afrika Mashariki.

Wakati tunaendelea kujitafakari na kurudisha nguvu ili kuinua tena sekta ya filamu, ni lazima tujifunze kutoka kwenye waandaaji na wasanii walioshiriki kwenye filamu hii ya Watu Wote/ All Of Us.

Tanzania tuna matukio mengi, tunaacha yanapita bila kuyatendea jambo kwenye filamu na tunabaki kuzalisha filamu zenye maudhui ya mapenzi yaliyowachosha mashabiki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles