25.5 C
Dar es Salaam
Saturday, May 18, 2024

Contact us: [email protected]

Fidel Castro kiongozi mtata atayekumbukwa kwa ujamaa wake

fidel-castro-speaks

Fidel Alejandro Castro (90) alikuwa kiongozi mwenye utata alisifiwa na wafuasi wake kama kiongozi wa ujamaa, askari mwanasiasa ambaye aliirudisha Cuba mikononi mwa watu.

Lakini alikabiliwa na shutuma kwa kuwanyamaziaha wapinzani wake kwa njia ya mateso na kwa kuwa na sera ambazo ziliporomosha uchumi wa Cuba.

Fidel Alejandro Castro Ruz alizaliwa tarehe 13 Agosti 1926, nje ya ndoa ya familia ya mkulima, Angel María Bautista Castro y Argiz, ammbaye alihamia Cuba kutoka Uhispania.

Mama yake , Lina Ruz González alikuwa kijakazi aliyefanya shughuli za shamba ambaye baadae alikuwa mpenzi wa baba yake ,na baadae ,baada ya kuzaliwa kwa Fidel, akawa mkewe.

Castro alisoma katika shule ya kikatoliki mjini Santiago kabla ya kujiunga na chuo kinachoendeshwa na makasisi wa Jesuit- kilicho El Colegio de Belen jijini Havana.

Hata hivyo, alishindwa kimasomo , na badala yake alipendelea kutumia muda wake mwingi katika shughuli za michezo.

Ilikuwa wakati anasomea sheria katika Chuo Kikuu cha Havana kati kati ya miaka ya -1940s ndipo alipokuwa mwanaharakati wa siasa, na kuimarisha ujuzi wake wa kuzungumza. 

Castro alikuwa miongoni mwa watu waliopanga njama za mapinduzi ya kumg’oa madarakani Rafael Trujillo, kiongozi wa mrengo wa kulia wa Dominican Republic , lakini jaribio hilo lilishindwa baada ya na Marekani kuingilia kati.

Mwaka 1948 Castro alimuoa Mirta Diaz-Balart, mtoto wa mwanasiasa tajiri nchini Cuba. 

Aliamini matatizo ya Cuba ya kiuchumi yalikuwa ni matokeo ya ubepari usioweza kudhibitiwa ambao unaweza kutatuliwa tu kwa mapinduzi.

Baada ya kuhitimu masomo Castro alizindua shughuli za kisheria lakini zilishindwa kufanikiwa na aliendelea kuingia katika mzozo wa madeni.

Alisalia kuwa mwanaharakati wa kisiasa, akishiriki katika misururu ya maandamano ya mara kwa mara ya ghasia.

Baada ya kushindwa kisheria, Castro alibuni shirika lililoitwa The Movement, lililoendesha shughuli zake kisiri kwa lengo la kuung’oa madarakani utawala wa Batista.

Cuba palikuwa mahala pa watu matajiri kujivinjari, na nchi iliongozwa na kiasi kikubwa na magenge ya wahalifu . Ukahaba ,wacheza kamali na walanguzi wa mihadarati vilikithiri. 

Baada ya kujaribu kufanya mapinduzi,  Castro alihukumiwa kifungo cha miaka 15 jela . Baadae aliachiliwa huru kufuatia tangazo la huruma la jumla la mwezi Mei 1955 baada ya kutumikia kifungo hicho kwa miezi 19 tu katika mazingira bora kiasi.

Katika kipindi hiki kifupi gerezani alimtaliki mkewe na kujiimarisha zaidi katika sera za kimaxist.

Kutokana na Batista kuendela kuwakamata wapinzani wake , Castro alitorokea Mexico kuepuka kutiwa nguvuni . Huko alikutana na mwana mageuzi kijana aliyeitwa Ernesto “Che” Guevara.

Mnamo mwezi Novemba 1956, Castro alirejea Cuba akiambatana na wanajeshi 81 kwenye ndege iliyokuwa na uwezo wa kubeba watu 12 pekee.

Makao makuu ya chama yalitafuta hifadhi katika milima ya Sierra Maestra . Kutoka kwenye ngome hii Castro alizingua vita vya msituni dhidi ya utawala wa Havana.

Tarehe 2 Januari, 1959, jeshi la waasi likaingia katika mji mkuu wa Cubanna Batista akatoroka.

Mamia ya wafuasi wa zamani wa Batista walinyongwa baada ya kesi ambazo wageni wengi waliziona kuwa hazikuwa za msingi. 

Serikali mpya ya Cuba iliahidi kurejesha ardhi kwa watu na kulinda haki zao. 

Castro mara nyingi alikuwa akisisitiza kwamba fikra zake zilikuwa ni bora zinajali kwanza maslahi ya watu wa Cuba.

Mnamo 1960, Fidel Castro aliwapatia uraia wamarekani woote waliokuwa wanamiliki biashara katika kisiwa hicho.

Kujibu hatua hiyo, utawala wa Washington ulimuwekea vikwazo vya kibiashara vilivyo tarajiwa kudumu kwa karne ya 21.

Castro alidai kuwa alilazimishwa kuingia katika mikono ya muungao wa Usovieti na kiongozi wake , Nikita Khrushchev, ingawa baadhi ya wachanganuzi walisema aliingia katika muungano huo USSR kwa utashi wake mwenyewe.

Iwe sababu yoyote ile, taifa la Cuba liligeuka kuwa uwanja wa mapamabano ya vita baridi vya dunia.

Mwezi Aprili 1961, Marekani ilijaribu kuipindua serikali ya Castro kwa kuwapatia mafunzo wanajeshi binafsi wa Cuba waliokuwa wakimbizi ili kuvamia kisiwa hicho. 

Fidel Castro alikuwa ameonja malaka kwa njia ya damu kwa hivyo asingeweza kuwasamehe.

Mwaka mmoja baadae, ndege za uchunguzi za Marekani ziligundua makombora ya Usovieti wakati zilipokuwa njiani kuelekea maeneo ya Cuba.

Dunia ilishtushwa na uwezekano wa kutokea vita vya nuklia. 

Mataifa yenye nguvu duniani yalibaki kushuhudia kinachoendelea lakini ni rais Khrushchev pekee ambaye aliweza kuchukua hatua kwanza na kuondoa makombora. 

Fidel Castro, hata hivyo , alikuwa tayari ni adui wa Marekani namba moja. Maafisa wa ujasusi wa Marekani CIA walijaribu kumuua mara kadhaa , katika kisa kilichojulikana kama. 

Muungano wa Usovieti ulimwaga pesa ndani ya Cuba. Ulinunua mavuno ya sukari inayozalishwa kisiwani humo na meli zake kurejea na zimesheheni na bidhaa nyingine, kama vile chakula kilichokua kinahitajika ili kukabiliana na vikwazo vya Marekani vya biashara.

Licha ya utegemezi wa msaada kutoka mataifa ya Usovieti , Castro aliiongoza Cuba kuwa taifa jipya lisilokuwa na mafungamano yoyote.

Hata hivyo, aliegamia hasa Afrika, ambako alituma majeshi kuunga mkono wapiganaji wa msituni waliokuwa na sera za kimaxist katika nchi za Angola na Msumbiji.

Akiwa bado chini ya vikwazo vya Marekani na kukatwa kwa huduma muhimu za mataifa ya Soviet , uhaba wa kudumu wa bidhaa na ukosefu wa akiba ya bidhaa vilidhihirika ndani ya Cuba. 

Taifa ambalo Fidel Castro aliita lililoendelea zaidi duniani, hali ya maisha ilikuwa mbaya.

Hata hivyo Cuba ilirekodi baadhi ya mafanikio ya kufurahisha ndani ya nchi. Huduma bora za matibabu zilitolewa bure kwa wote , na viwango vya vifo vya watoto wachanga wa vililinganishwa na vile vya mataifa tajiri duniani.

Katika miaka iliyofuata , Castro alionekana mtulivu . Mwaka 1998 alitembelewa na Papa John Paul II, jambo ambalo halingeweza hata kufikiriwa miaka mitano ya awali.

Wakati huo Papa aliilaumu Cuba kwa ukiukaji wake wa haki za binadamu , na kumuaibisha Castro mbele ya vyombo vya habari vya dunia.

Fidel Castro alikuwa amebuni utambulisho wake kama mjamaa wa Caribbean ambao kwa miaka kumi iliyopita , alilazimika kuukumbatia , pole pole alianzisha mabadiliko machache ya biashara huria ili kulinda mageuzi yake.

Tarehe 31 Julai 2006,siku chache tu kabla ya maadhimisho ya mwaka wake wa 80 wa kuzaliwa, Castro alikabidhi mamlaka ya muda kwa Raul baada ya kufanyiwa upasuaji wa dharura wa utumbo.

Afya yake iliendelea kudhoofika. Mapema mwaka 2008, Castro alitangaza kwamba hatakubali nyadfa za urais na amiri jeshi mkuu katika mkutano kuu ujao wa kitaifa.

Alijiondoa kwa kiasi kikubwa katika maisha ya umma , huku akiandika taarifa zilizochapishwa katika vyombo vya habari vya kitaifachini ya kichwa cha habari…Tathmini ya maisha ya amir Fidel.

Wakati wa Cuba wengi bila shaka hawakumpenda Castro, wengine walimpenda kwa dhati . Walimuona kama David ambaye aliweza kukabiliana na Goliath wa Marekani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles