25.6 C
Dar es Salaam
Sunday, January 5, 2025

Contact us: info@mtanzania.co.tz

Fid Q: Najuta kutoa albamu mapema

fid-qNA CHRISTOPHER MSEKENA

MSANII wa muziki wa hip hop nchini, Farid Kubanda ‘Fid Q’ amesema anajutia kutoa albamu yake ya kwanza inayoitwa ‘Vina Mwanzo Kati na Mwisho’ mapema kabla mfumo wa kutumia CD kuingia Tanzania.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Fid Q alisema kuwa mfumo wa  kutumia kanda ulifanya albamu hiyo kuwafikia mashabiki wachache tofauti na malengo aliyojiwekea na anaamini angetumia CD kazi yake ingewafikia wengi.

“Muda mwingine nawaza albamu yangu ningeitoa kipindi ambacho CD zimeanza kutumika ingewafikia wengi zaidi, kwa sababu kanda ni mfumo ambao ulikuwa unapunguza kasi ya usambazaji wa kazi zetu,” alisema Fid Q.

Aliongeza kuwa alitaka kutoa nakala laki tatu za CD lakini msambazaji alikataa akataka atoe nakala laki moja peke yake, kwa hiyo kilichofanya ajutie ni kwamba albamu hiyo haikuwa kwenye mfumo wa CD, hivyo haikuwafikia watu wengi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
593,000SubscribersSubscribe

Latest Articles