27.2 C
Dar es Salaam
Friday, September 30, 2022

Diamond amshinda Miss Dunia tuzo za MTV-EMA

hhjNA MWANDISHI WETU

MKALI WA muziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul, maarufu kama Diamond Platnumz, amempiku mwigizaji na mwanamuziki aliyewahi kuwa mrembo wa dunia mwaka 2000, Priyanka Chopra, kwenye tuzo za MTV Europe Music Awards (MTV-EMA).

Tuzo hizo zilizofanyika nchini Italia usiku wa kuamkia jana, wawili hao walikuwa wanachuana kwenye kipengele cha ‘Best Worldwide Act’, tuzo ambayo ilikuwa na ushindani mkubwa kutoka kwa nyota wengine wa muziki kutoka mataifa ya Australia, New Zealand, Ulaya, Latin America na Marekani Kusini.

Diamond alidai tuzo hiyo ni muhimu na si ya kwake peke yake.

“Tuzo hii siyo yangu ni yetu sote, kwa sababu bila kura zenu nisingeweza kushinda kutokana na ushindani uliokuwepo kwenye kipengele hiki,” alishukuru Diamond.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,327FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles