24.2 C
Dar es Salaam
Sunday, May 19, 2024

Contact us: [email protected]

Federer kuwa nje ya uwanja mwezi mmoja

FedererZURICH, USWISI

NYOTA wa mchezo wa tenisi ambaye anashika nafasi ya tatu kwa ubora duniani, Roger Federer, atakuwa nje ya uwanja kwa mwezi mmoja kutokana na kusumbuliwa na goti.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 34, ambaye ni mshindi mara 17 wa Grand Slam, aliumia wakati wa mashindano ya wazi ya Australia huku akiondoshwa katika hatua ya nusu fainali na Novak Djokovic wiki iliyopita.

“Ninashukuru Mungu kwamba ninaendelea vizuri, ila ninasikitika kwamba nitakuwa nje ya uwanja kwa muda wa mwezi mmoja.

“Hata hivyo, daktari wangu amenithibitishia kwamba nitafanyiwa upasuaji na nitakuwa vizuri baada ya muda mfupi, na mimi mwenyewe ninaamini nitarudi uwanjani muda mfupi ujao mara baada ya kufanyiwa upasuaji huo,” alisema Federer.

Fainali hizo za wazi katika michuano ya Australia, Djokovic alifanikiwa kuwa bingwa baada ya kumchapa mpinzani wake, Andy Murray kwa seti zote tatu.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
587,000SubscribersSubscribe

Latest Articles