Vidal avitupia lawama vyombo vya habari

0
709

arturo-vidal-accident-1MUNICH, UJERUMANI

KIUNGO wa klabu ya Bayern Munich, Arturo Vidal, amevitupia lawama vyombo vya habari nchini Ujerumani kwa kutoa taarifa kwamba mchezaji huyo aliingia mazoezini huku akinuka pombe.

Gazeti la Bild la nchini humu liliandika kwamba nyota huyo wa timu ya Taifa ya Chile, wiki iliyopita alikuwa mjini Qatar akiwa na klabu hiyo kwa ajili ya mazoezi, ila aliwashangaza wachezaji wenzake kwa kuwa alikuwa ananuka pombe mazoezini.

Hata hivyo, mchezaji huyo kupitia akaunti yake ya Instagram amekanusha uvumi huo na kusema kwamba ni habari za uongo.

“Natumia nafasi hii kupinga kauli ambayo imeandikwa na gazeti moja la nchini Ujerumani kwamba niliingia uwanjani nikiwa nanuka pombe.

“Hata hivyo, mwanasheria wangu analifuatilia jambo hilo kwa ajili ya kulichukulia hatua za kisheria kutokana na kuchapisha habari ambazo si sahihi.

“Nina asilimia 100 kwamba ninajitolea kikamilifu katika klabu yangu na kwa sasa tunajiandaa na mapumziko ambayo ni muhimu sana kwa upande wetu. Nawashukuru mashabiki wangu kwa ushirikiano mkubwa ninaoupata,” alisema Vidal.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here